Imeripotiwa mwanzoni mwa wiki iliyopita Samsung waliwakasirisha Microsoft baada yakugundulika kwamba walihusika kuweka kaprogramu katika kompyuta zake ambacho kinaingilia ufanyaji kazi wa programu muhimu ya kusasisha (update) kompyuta zinazotumia Windows inayofahamika kama Windows Updates.
Sakata hili liligundulika baada ya kampuni ya WAVLY kupata shida katika kompyuta zao (ambazo zimetengenezwa na Samsung) juu ya ‘updates’ za Windows, hali hii ilipelekea wao kuwasiliana na watoa msaada wa Windows ambao ndio wakagundua kwamba kinacholeta tatizo katika kompyuta hizo kuliiingia katika kupitia programu spesheli ya Samsung.
Samsung kupitia programu yao waliyoiweka kwenye baadhi ya kompyuta zao ilikuwa na lengo la kuzuia Windows kushusha na kupakua misasisho mipya (updates) kutoka Microsoft katika kompyuta husika. Programu hiyo inachofanya ni ku’reset’ mpangilio (Setting) wako wa Windows Update na kufanya uwe katika chaguo la kutafuta misasisho mipya (updates) lakini kukulazimu wewe mtumiaji kuchagua misasisho ya kushusha (Check for updates but let me choose whether to download or install them”). Programu hiyo kutoka Samsung hufanya ‘reset’ kila mara ambapo Windows inazima hivyo haijarishi ni mara ngapi utafanya mabadiliko katika mpangilio huo pindi unapozima kompyuta basi yenyewe ita reset mpangilio huo.
Mwanzoni Samsung ambayo ni kampuni ya kikorea walipoulizwa juu ya hili tarehe 24/06/2015 walisema kwamba wanafuatilia malalamiko hayo lakini badae siku hiyo hiyo samsung wakabadirika na kusema kwamba hawajafanya kosa lolote katika suala hilo, hata hivyo baada ya misuguano na kutupiana lawama Ijumaa tarehe 26 makampuni hayo mawili yalifikia muafaka ambapo Samsung ilikubali kuondoa programu hiyo iliyokuwa inaleta matatizo.
No Comment! Be the first one.