Ni wazi kwa sasa vifaa vya kujikunja ni vingi sana na kwa sasa kuna makampuni mengi ambayo yana simu janja ambazo ziko katika muundo huo lakini Apple bado hawana vifaa vya aina hii.
Kwa upande wa Samsung ndio ambao wameliteka soko hili katika simu janja, makampuni mengine mengi tuu yapo ambayo yana simu za aina hii—vipi kuhusiana na Apple?
Mpaka sasa Apple –wapinzania wakubwa wa Samsung—bado hawajaingiza simu za aina hii katika soko pengine ndio moja ya sababu inayoifanya kampuni ya Samsung kuzidi kuwa namba moja.
Samsung wanaamini kuwa kampuni ya Apple itaweza kutangaza kifaa chake cha kwanza cha kujikunja ifikapo mwaka 2024 lakini kifaa hicho hakitakua ni iPhone.
Inasemekana kifaa hicho kitakua ni iPad au MacBook, lakini ukiachana na hili Samsung ambalo wanalidhania wao hawajaweka wazi kuhusiana na kifaa chochote cha kujikunja kutoka kwao.
Mwezi septemba mwaka huu, kuna taarifa zilitoka kwamba kampuni ya Apple waliwataka LG na Samsung kuwatengengezea vioo vya OLED vya kukunjika — pengine hii inaweza ikawa ni moja kati ya ishara ya jambo hili kuwezekana.
Soko la simu janja za kujikunja bado linakua kwa kasi sana, japokua katika soko hakuna simu nyingi za mfumo huu lakini nia nyingi kwa makampuni mengi zimeonekana wote wakitaka kuingia katika soko hili.
Unaweza ukawa unajiuliza kwanini Samsung anahisi jambo hili litatokea mpaka kufika 2024, lakini kumbuka kwamba Apple huwa inanunua vipuri vya vifaa vyake kwa makampuni mengi tuuu Samsung ikiwa ni moja kati ya makampuni hayo.
Ningependa kusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini wewe unadhani wao Apple wataingia na iPhone, iPad au MacBook katika soko la kvifaa vya kujikunja?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.