Wapenzi wa simu za Samsung hawakuwa wanajua kuhusu ujio Samsung Galaxy J7 Prime 2 lakini sasa ni wazi kwamba simu hiyo ilizinduliwa kimya kimya nchini India.
Haijulikani kwanini Samsung hawakutaka kuufahamisha ulimwengu kuhusu ni lini na wapi simu hiyo ingezinduliwa lakini watu wakashangaa tu imeanza kuunzwa nchini India. Swali ambalo najua utakuwa unajiuliza ni “Samsung Galaxy J7 Prime 2 ina sifa zipi?”. Samsung Galaxy J7 Prime 2 ina sifa zifuatazo:-
>Prosesa na Kioo (display)
Prosesa ya kwenye Samsung Galaxy J7 Prime 2 ni octa-core Exynos 7 Series na 1.6GHz ambayo inaifanya simu kuwa na kasi wakati mtu anapoitumia. Kioo chake kina ukubwa wa inchi 5.5 chenye uwezo wa full-HD (1080×1920 pixels).
>Programu Endeshaji na Betri
Imeelezwa kuwa simu hii inatumia mfumo endeshi wa Android ingawa haijawekwa wazi ni toleo gani la Android Samsung Galaxy J7 Prime inatumia; wengi wanaeleza kuwa ni kuanzia Android 7.0 na kuendelea.
>Diski uhifahi na RAM
Simu janja nyingi za miaka ya karibuni ni nadra sana kukuta ikija na diski uhifadhi yenye ukubwa wa GB 16; ni kama muda wake umepita 😆 😆 . Samsung Galaxy J7 Prime 2 ina GB 32 ya diski uhifadhi huku ikiwa na uwezo wa kuweka ujazo wa ziada wa mpaka GB 256. Simu ina GB 32 ya uhifadhi basi na RAM ni muhimu kuwa kubwa hivyo simu hii ina RAM ya GB 3.
>Kamera na Betri
KIvutio cha watu wengi duniani wanaotumia simu janja ni katika kipengele hiki na kama kampuni inataka simu husika isifanye vizuri kwenye mauzo basi isiweke kamera bora au betri lenye uwezo mkubwa. Kwenye Samsung Galaxy J7 Prime 2 ina kamera 2 (nyuma na mbele) na zote zina MP 13 huku betri yake ikiwa na 3300mAh.
>Bei na Mengineyo.
Nchini India inauzwa kwa $215|Tsh.483,750 lakini usitegemee kuwa utanunulia kwa bei hiyo ikifika Tanzania. Samsung Galaxy J7 Prime ina sehemu moja tu ya kuweka laini; tena laini ndogo. Sifa zake nyingine ni pamoja na Wi-Fi 802.11 b/g/n, GPS, Bluetooth v4.1, sehemu ya kuchomeka spika za masikioni, ina uzito wa gramu 170, inakubali 3G na 4G pia ina teknolojia ya ulinzi wa kutumia alama ya kidole iliyopo nyuma ya simu.
Huo ndio undani wa Samsung Galaxy J7 Prime 2 ambayo bado haijaanza kuuzwa kwingineko duniani isipokuwa India tu na kama utaihitaji basi itakubidi utembelee tovuti Samsung na ubofye kwenye kipengele cha “Notify me” ili uweze kujulishwa mara tu zitakapoanza kupatikana.
Vyanzo: Gadgets 360, The Indian Express
One Comment
Comments are closed.