Kutoka SanDisk hii ndio itakua memori kadi yenye ujazo mwingi kuliko zote duniani, maana hii ni ya kipekee. Kumbuka ujazo huu ni mwingi kulinganisha na hata ule ambao upo kwenye baadhi ya Laptop.
Tarehe 20 mwaka huu (2016) kampuni nguli duniani linalojihusisha na maswala mazima ya ujazo wa uhifadhi katika vitu vya kidigitali. Kampuni hiyo ijulikanayo kama Western Digital Corporation (WDC) ilijiweka kifua mbele na kutangaza kuhusu memori kadi hii katika tamasha lijulikanalo kama Photokina huko nchini Ujerumani.

Jina la memori kadi hiyo ni ‘The SanDisk Extreme Pro SDXC UHS-I’ na ujazo wake ni ‘terabyte’ moja – huu ni ujazo wa juu kabisa kwa sasa – kumbuka ujazo huu kwa sasa ndio unaosemekana kuwa wa mwisho. Pengine watu wanafanya kazi kubwa ili kutengeneza vifaa ambavyo vitapita ujazo huo.
Kwa kampuni hili ni jambo jema kabisa kwani wametoka mbali, kumbuka walianza kutengeneza memori kadi zenye ujazo wa uhifadhi mwaka 2000 ambapo walitengeneza yenye ujazo wa MB 64 na leo wanakuja na 1 TB!
Ni maendeleo makubwa sana kwao, kampuni limesema limeamua kutengeneza Memori kadi kubwa kiasi hicho kutokana na muda kubadilika na pia wateja wao kwa muda mrefu wamekuwa wakihitaji memori kadi ya namna hiyo.
SOMA PIA: Western Digital Mbioni Kuinunua SanDisk Kwa Dola Bilioni 19!
SOMA PIA: Flash Diski Yenye Umbo Dogo Kuliko Zote Duniani kutoka SanDisk
Kumbuka memori kadi za namna hii ni lazima hasa katika kamera, kumbuka sasa hivi kamera nyingi zinazotoka zinakuja na uwezo wa 4K na hata 8K inakuwa, kumbuka pia aina hizi za video zinakula ujazo mkubwa sana. Lakini kampuni imeliona hilo kwa jicho la tatu.

Ni wazi kabisa kwamba kwa dunia ya sasa, ujazo huo wa uhifadhi katika memori kadi unahitajika sana. Ukiachana na mambo ya 4K au hata 8K kumbuka pia bado kuna mambo mazima ya video za ‘VR (virtual Reality), video za 360’ na mambo mengine mengi ambayo kwa kiasi kimoja au kingine yanahitaji ujazo wa uhifadhi mkubwa.
SanDisk haikusema lini memori kadi hiyo itaanza rasmi kuuzwa na pia hata bei yake haikuwekwa wazi. Cha msingi ni kwamba bidhaa tayari ipo, hivyo basi tukae mkao wa kula wakati tunaisubiria hii
Niandikie hapo chini sehemu ya comment, je ulishawahi fikiria kama itakuja memori kadi yenye ujazo wa uhifadhi wa TB 1? Ningependa kusikia kutoka kwako.