Tangia kipengele cha View once (kama ukitaka ulichotuma kionekane mara moja) kutoka ndani ya mtandao wa WhatsApp kumekua na mapokezi mengi na ya hali ya juu….
Licha ya mapokezi kuwa ya juu sana, lakini bado kuna vyanzo mbalimbali vilitoa mawazo yao kuhusiana na kipengele hicho, ni kweli kipengele ni kizuri lakini mtumaji anakua hana uhakika kwamba kitu alichotuma hakitaonwa tena.
Ni wazi kuna njia nyingi sana za kuona kitu hiko ikiwemo na ile ya Ku’Screen Shot, WhatsApp waliliona hilo na kwa sasa wamefanya maboresho ambayo kwa namna moja au nyingine hairuhusu jambo hilo katika kipengele husika.
📝 WhatsApp beta for Android 2.22.22.3: what's new?
WhatsApp is releasing screenshot and screen recording blocking for view once images and videos to some beta testers!https://t.co/KJC3jRTlXf pic.twitter.com/9uxPzfTdc6
— WABetaInfo (@WABetaInfo) October 3, 2022
Pengine kipengele hiki kitaanza kupatikana kwa watumiaji wa simu za Android maana kwa sasa toleo la majaibio ya kipengele hiki kinapatikana huko. Kwa watumiaji wa iOS Pengine na wao wataanza kupata kipengele hicho huko mbeleni kabisa au vilevile wanaweza pata pamoja na wa Android.
Kilichotokea hapa ni kwamba mtandao wa WhastApp utakua umejiimarisha kabisa katika kipengele cha kiulinzi na kiusalama na hvyo kumzuia mtu kuweza kuchukua hata Screen Shot ya kitu ambao umeuamuru mtandao umuonyeshe mara moja tuu.
Chanzo WABetaInfo
Soma Kila Kitu Kuhusiana Na Mtandao Wa WhatsApp >>>>>>>>>HAPA<<<<<<<<<
Ningependa kusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini katika eneo la comment, je hii umeipokeaje? Je unaona kampuni inafanya sawa? Lakini ushawahi fikiria maana mtu anaweza akatumiwa kitu mara moja lakini akachukua simu nyingine na kukirekodi au kukipiga picha bila muhusika kujua?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.