Baadhi ya watumiaji wa WhatsApp wameshaonja shubiri ya kufungiwa akaunti zao za WhatsApp ingawa si ile WhatsApp inayotambuliwwa rasmi na Facebook. Sasa inawezekana kufungiwa akaunti ya WhatsApp kwa watumiaji wote.
Takribani mwezi mmoja uliopita WhatsApp upande wa iOS walianza kufanyia kazi kipengele kipya cha ndani kwa ndani kuweza kupitia akaunti iliyozuiliwa kutumika (banned). Mtumiaji anakuwa na uwezo wa kutuma ripoti moja kwa moja kwenda kwa WhatsApp ili akaunti yake iweze kupitiwa na hatimae kufunguliwa. Mbali na hilo mtu anaweza kuweka maelezo akifafanua kilichotokea kabla ya akaunti kufungiwa pamoja na mambo mengine.
Kimsingi maboresho hayo yameonekana kufika kwenye WhatsAp Beta toleo namba 2.21.18.5 ambapo akaunti ya mtu inaweza kufungiwa kutokana na sababu mbalimbali mathalani unaweza ukajikuta umeingizwa kwenye kundi ndani ya WhatsApp bila idhini yako na hatimae ukafungiwa kutumia programu tumishi yenye wateja wengi duniani kote kutokana na kufanya ndivyo sivyo.
Kwenye kuomba kuna mawili; kukubaliwa au kukataliwa
Ndio, haimaanishi kuwa ukipeleka ombi lako kwa WhatsApp wapitie akaunti yako na kuona iwapo ulistahili kweli akaunti yako kufungiwa basi majibu yatakuwa mazuri siku zote la hasha! Inaweza ikatokea ombi lako likakataliwa hivyo hutaweza kutumia akaunti yako ya WhatsApp na kama ombi lako litakurudi na majibu chaya basi utarudishiwa uwezo wa kuendelea WhatsApp.
Kwa sasa kipengele hicho kipo katika hatua ya majaribio hivyo ni baadhi ya watu tu (wanaotumia toleo tajwa) ndio wameyaona maboresho hayo. Haijulikani ni lini kipengele hicho kitapatikana kwa wote.
Tunachoweza kusema ni kuhakikisha unaboresha WhatsApp kila mara unapoona kuna taarifa inayokutaka kufanya hivyo.
Chanzo: WaBetaInfo
naomba kufunguliwa kutumia whatsapp kwa namba 0716300600 nilikuwa natumia yowhatsapp bila kujua kuwa hazitambuliki, naomba nifunguliwe ili nitumie whatsapp ya kawaida.
Kutumia matoleo yasiyorasmi ya Whatsapp ni hatari kwa usalama wa data zako. Ukifungiwa hakuna cha kufanya, unaweza jaribu tena baada ya mwezi au miezi 3, inachukua muda akaunti kuruhusiwa tena ikishafungiwa