Instagram imweka wazi kipengele hichi cha uwezo wa kushusha Reels zote ambazo zinapatikana kwa akaunti ambazo kila mtu anaweza kuziona (public accounts).
Kumbuka instagram kuna akaunti za aina mbili, ile ambayo kila mtu anaweza kuingia (public account) na ile nyingine ambayo mpaka utume ombi (private account) na zote zina huduma hiyo ya Reels.
Hili linawezekana kwa akaunti ambayo mtu yeyote anaweza kuingia, na hili limefanyika makusudi ili kulinda baadhi ya video ambazo pengine mtu asingependa zizagae kwa macho ya watu pasipo watu ambao amewapa ridhaa hiyo.
Kipengele hiki wapinzani wao TikTok wanacho tokea muda sana na watumiaji wake wamekua wakikifurahia maana kinawafanya kuweka/kusambaza video hizo katika mitandao mingine ya kijamii.
Kipengele hiki kwa sas akinapatikana kwa watumiaji wote wa Android au hata iOS na kingine kumbuka kipengele hiki kilianza kutumika tangia mwezi wa saba lakini kilikua kikipatikana marekani tuu.
Kingine ni kwamba wenye akaunti watakua na uwezo wa kuwezesha kwamba ni nani ashushe video hizo (Reels) za kwenye akaunti yao kwa kuingia katika settings.
Ningependa kusikia kutoka kwako, je umeshaanza kutumia kipengele hiki? Unakionaje niandikie hapo chini katika uwanja wa comments
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.