Kwa sasa Shazam imerahisisha mno katika swala zima la kutambua nyimbo fulani na hili linafanyika kwa njia ya kutumia spika za masikio tuu.
Shazam ilinunualiwa na Apple kwa mamilioni ya dola za kimarekani na kampuni ya Apple mwaka 2017, kusoma vizuri kuhusiana na hili gusa >>HAPA<<
Kutokana na toleo jipya (update) ya Shazam ambayo imetoka inawezesha utambuzi wa nyimbo kupitia katika spika za masikio zile za nyaya au zile za Bluetooth.
Kumbuka hapo mwanzo kabisa ila kutambua nyimbo fulani ilikua inakulazimu kutumia vinasa sauti vya simu bila kutumia kinasa sauti cha kupachika au kuunganisha kama vile spika za pembeni.
Pata picha kama uko katika mitandao ya TikTok, Instagram na YouTube utakua hauna haja ya kutoa spika za masikio ili kutambua nyimbo fulani.
Ufanyaji kazi kipengele hiki kipya hauna tofauti sana cha kufanya ni kuwasha App yako ya Shazam na kisha kwenda katika App inayopiga ili kutambua wimbo husika.
Kwa kufanya hivyo hapo utaona alama ya spika za masikio ikiashiria kwamba kwa wakati huo utambuzi unafanyika kupitia spika hizo.
Utambuzi ukikamilika utapata taarifa ambayo inakuarifu hivyo na hata kama utambuzi usipofanikiwa bado utapata taarifa hiyo.
Ningependa kusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini katika eneo la comment je unaipa asilimia ngapi App ya shazam kwa kuja na kipengele hiki?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.