Shazam ndio mtandao namba moja ambao unasaidia watu kutambua majina na taarifa nyingi za mziki ambao unaimbwa.
Ni mara ngapi umeshawai kusikia mziki unapigwa lakini hujui nani kauimba na hata pengine mashairi yake huyajui vizuri? Shazam inaweza kuwa ni mkombozi wako katika hili.
Shazam ilinunuliwa na Apple na kwa sasa Apple yenyewe imetoa taarifa kwamba itatoa sasisho la App hiyo ambalo litaweza kusaidia watu kujua miziki kutokea katika mitandao ya kijamii ya YouTube, Instagram na hata TikTok.
Unaweza ukajiuliza sasa kwa YouTube inakuaje? Iko hivi unaweza ukawa unaangalia video ambayo sio ya mziki pengine inaweza ikawa ni kipindi na kwa nyuma ukawa unasikia sauti ya mziki.
Kwa kupitia huduma ya Shazam unaweza ukapata taarifa zote za muziki huo na sana sana ikiwa ni kwamba hujawekewa taarifa zozote za mziki huo katika eneo la maelezo (description) katika mtandao wa YouTube.
Uzuri ni kwamba huduma hii itakua na uwezo wa kufanya kazi juu ya App husika (Instagram, YouTube au TikTok).
Cha kufanya ni kwamba gusa App ya Shazam ili kuwasha na kisha rudi katika App husika ili kupata matokeo ya tafuto husika.
Kwa sasa huduma hii inapatikana katika vifaa vya iOS tuu japo huduma ya Shazam inapatikana pia katika Android lakini huduma hii bado haijaanza kupatikana katika Android.
Ni wazi kwamba kuna muda utafika huduma hii itaanza kupatikana kwa watumiaji wote wa App hiyo katika vifaa tofauti tofauti.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment je unadhani ni sahahi kwa huduma hii kuanza kupatikana kwa wale wa iOS tuu?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.