Duuh! Huu ndio umekua mwaka wa mabadiliko makubwa kwa mtandao wa Instagram ukilinganisha na miaka mingine iliyopita.
Kumbuka mwaka huuu vitu kama logo, stories, kukuza picha, matangazo n.k vilianzishwa katika mtandao huu ili kuhakikisha tuu watu wanaufurahia zaidi na zaidi.
Sasa baada tuu ya kuongeza kipengele cha notification ambazo zinaonyesha picha, Instagram imeweka wazi kipengele kingine ambacho kinamruhusu mtumiaji wa mtandao huo kuweza ku’like comment au kuizima na vile vile hata kuwaondoa followers.
Hili watalifaidi wale ambao watasasisha vifaa vyao vya iOs au Android kwenda katika toleo jipya zaidi.
Ngoja Nkuonyeshe Jinsi Mambo Yatakavyo Kuwa
- Ku Like Comment
Watumiaji watakuwa na uwezo wa kuweza ku’like comment za watu. Kama comment ikikurufahisha na hujisikii kuijibu au uko bize kidogo na majukumua unaweza ukagonga like tuu na mambo menginr yakaendelea. Kitu ambacho utatakiwa kufanya ni kobofya mara mbili (Kama wakati una like picha) katika kile kialama cha moyo pembeni ya comment ya mtu.
- 2.Kuondoa/Kufuta Follower
Kumbuka hapo mwanzo njia pekee ambayo ilikuwepo ya kumuondoa Follower ilikua ni kupitia kumblock. Kwa sasa mambo yameboreshwa na mtu unaweza fanya jambo hili kwa urahisi kabisa baada ya kipengele cha ‘Remove’ kuongezwa
Kwa sasa watu ambao wana akaunti za ‘Private’ ndio ambao kipengele hiki kimewapendelea sana. Pembeni ya list ya followers wako utoana kuna vidoti, ukivifungua ndipo unaweza ukamuondoa mtu usiye mtaka katika list yako.
- 3. Kuzima Comment
Kwa sasa instagram inakuwezesha kuzima comment, tena hii ni sehemu zote ni kwa post mpya na zile za zamani.. NImeshasikia wasanii wengi wa Tanzania wanalalamika kuwa wanatukanwa sana katika mtandao wa Instagram pengine kipengele hiki ndio mkombozi wao.
Wakati unampango wa kuweka picha mpya katika mtandao wa Instagram ukishafika katika eneo la kuandika ‘caption’ kwa chini kuna eneo la “advanced Settings” na ukiingia humo ndipo unaweza kuzima comment hizo
Instagram inafanya juu chini ili kuhakikisha kuwa watumiaji wake wanapata vingi vizuri kuliko vile ambavyo mwanzo walikuwa wana vitegemea. Nini kingine unahisi kikawa ni kipengele kipya katika siku za usoni?