Pushbulet, ile app inayokupa taarifa kutoka kwenye simu yako kupitia kompyuta inaweza kutumika kikamilifu sasa kwa ajili ya ujumbe mfupi. Kabla ya sasa, ulikuwa unaweza kupokea ujumbe mpya na kuujibu papo-kwa-hapo na kutuma ujumbe mpya tu, bila kuona mazungumzo yote. Kwa kipengele kipya ambacho pushbullet imeongezewa, mtu unaweza kufanya mazungumzo na watu kadhaa kiurahisi bila ya kuhitaji kuinua simu.
Kwenye kurasa ya pushbullet, kwenye kivinjari cha kompyuta na kupitia programu ya Windows na Mac, kipengele hiki kipya cha SMS utakipata upande wa kushoto kama ilivyooneshwa kwenye picha hapa chini. Hapo utaweza kuona na kutuma ujumbe wako. Unapobofya ‘send’, ujumbe wako unatumwa kupitia simu yako, ikimaanisha, itatumwa kwa namba yako ya simu.Hii yote inawezekana ukitumia sasisho jipya la pushbullet linalopatikana kwenye playstore sasa.
No Comment! Be the first one.