TikTok ni moja kati ya mtandao wa kijamii mkubwa kabisa na wenye nguvu kubwa sana kwa sasa ukilinganisha na mitandao mingi tuu.
Mara kwa mara mtandao wa TikTok umekua ukifanya maboresho kadha wa kadha katika kuhakikisha kuwa watumiaji wake wanapata kile wanachostahili.
Ni wazi kwamba mtandao huu ambao umejikita sana katika video na moja kwa moja kwa sasa mpinzani mkubwa ni mtandao wa YouTube.
Ni wazi kwamba mtandao wa TikTok kwa sasa umeweka kipengele ambacho kitaruhusu video za mpaka dakika 30 kuruka katika jukwaa hilo.
Kumbuka mara ya kwanza kabisa katika jukwaa hili video zilianza kuwa na dakika 1 na kisha kusogea mpaka dakika 3.
Halikuishia hapo bado dakika zilisogezwa mpaka kufikia 10 na kisha kuongezwa mpaka kufikia dakika 15.
![tiktok](https://www.teknolojia.co.tz/wp-content/uploads/2022/01/tiktok-5323005_1920.jpeg)
Kipengele hiki kimeanza kupatikana katika baadhi ya maeneo kwa sasa na kama wewe hujaanza kukitumia hakikisha una toleo jipya kabsia (update) kama bado huna budi kusubiri.
Kipengele hiki ni muhimu sana kwa waandaaji wa maudhui ambao wana mengi ya kuwasilisha kwa kupitia video moja.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment je hili unadhani limekaa poa? Usifikirie sana bando lako hahahahahaha!
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.