Kampuni ya Seagate watengenezaji wa diski za ukubwa mbalimbali wametangaza kuanza kuuza diski zenye ukubwa huo wa uhifadhi. Diski hizo zenye ukubwa wa takribani inchi 3.5 kwa sasa zinapatikana kwa ajili ya wateja wakubwa wa mashirika ya uhifadhi wa data kubwa zikitegemewa kuingia sokoni kwa watumiaji wengine ifikapo hapo mwakani.
Je diski za ukubwa gani wa juu zinapatikana kwa sasa?
Kwa sasa kama unauhitaji wa diski za uhifadhi mkubwa zaidi zinapatikana kwa kiwango cha cha juu cha Terabaiti 6 (6 Terabytes/TB). Wastani wa bei ya diski moja ya TB 6 ni takribani Tsh laki 5 kwa zile diski za ndani za kompyuta. Diski ya TB 5 inakaribia bei hiyo pia, wakati za TB 4 zinapatikana kwa bei kati ya laki 300,000 hadi 350,000/=
Ujio wa diski za TB 8 kutasaidia kwa sana kushuka kwa bei ya diski za TB 4, 5 na 6.
Je unaweza fikiria kutumia diski moja yenye ukubwa wa TB 8? Yaani kama unafilamu zenye ukubwa wa 800MB kila moja inamaanisha kuijaza utaitaji zaidi ya mafaili 1,250,000 kujaza diski hii moja. Ila kwa watumiaji kompyuta zao kwa ajili ya kucheza magemu makubwa basi diski ya TB 8 itakuwa inaitajika kwa sana tuu, kwani magemu mengi huchukua nafasi kubwa sana. Ila ata kwa matumizi hayo pia, kujaza diski ya TB 8 ni ishuuuuuu!
No Comment! Be the first one.