Miaka kama mitatu minne hivi iliyopita mtu asingefikiria kuna muungano kama huu ungeweza kutokea katika kuleta kifaa chochote kama tableti. Lakini umetokea.
Baada ya BlackBerry kununua kampuni moja ya teknolojia ya kiusalama zaidi ya Secusmart ya huko Ujerumani sasa wameshirikiana na kampuni ya IBM na Samsung na kuleta tableti iliyo kwenye kiwango cha juu kabisa cha kiusalama inayoenda kwa jina la SecuTABLET.
Tableti hiyo ambayo itaweza kutumiwa na vitengo muhimu vya kiserikali na makampuni au mashirika kama ya kibenki n.k ambayo ni muhimu masuala/data zake zitunzwe kwa usiri mara zote kuzilinda kutoka kwenye wizi wa kiintaneti – yaani ‘hacks’.
Tableti hii itatengenezwa kutumia toleo la Samsung Galaxy Tab S 10.5 na teknolojia ya ulinzi iitwayo ‘secure app wrapping’ kutoka IBM. Apps za kawaida kama vile Facebook, YouTube, Twitter na WhatsApp pia zinaweza kutumika bila wasiwasi wowote wa kiusalama.
Kampuni ya BlackBerry inajikita zaidi katika masuala ya teknolojia ya usalama na inasemekana imeanza kuona mapato yake yakikua zaidi taratibu. Kampuni ya teknolojia ya usalama ya Secusmart waliinunua mwezi wa kumi na mbili, 2014 na pia tayari kwa ushirikiano na Samsung, BlackBerry wametoa programu inayoweka ulinzi zaidi kwa simu na tableti za Samsung Galaxy inayotambulika kama ‘BlackBerry Enterprise Service 12’.
Bado hawajasema rasmi tableti hii ya SecuTABLET inataingia lini sokoni ila wameshaeleza ni itakuwa inauzwa bei ya juu zaidi kutokana na teknolojia iliyotumika na aina ya wateja wanaotegemewa kuitaji kifaa kama hichi.
No Comment! Be the first one.