Shaquille O’Neal ni mchezaji wa zamani wa ligi kuu ya kikapu inayojulikana kama NBA na aliweza kuchukua mataji mara 15 ya NBA All-Star, 4 ya NBA Champion, 3 Ya NBA Finals MVP na mengine mengi akiwa katika kikapu na sasa ni muwekezaji katika App na mambo mbalimbali.
Shaquille O’Neal pia ameweka wazi kwamba sio kama atafanya uwekezaji katika App hizo za masomo/elimu tuu bali atawekeza hata kwa zile ambazo zipo kwa ajili ya kubadilisha maisha ya watu.
Huyu ni moja kati ya watu maarufu na ni kwamba na pesa nyingi ambazo kwa sasa anajikita sana katika uwekezaji kwa namna zote hata zile za kupitia kwa watu.
Mpaka sasa yeye ndio mwekezaji mkuu katika App ya Edsoma ambayo itumia mfumo wa AI (Artificial Intelligence) ambayo imejikita katika kusaidia katika kusoma, elimu na mawasiliano kwa ajili ya watoto.
O’Neal mwenyewe ameweka wazi kwamba alisukumwa Zaidi baada ya kumsikiliza Jeff Bezos ambae ni miongoni mwa matajiri wakubwa kabisa katika dunia akisema kuwa ukiwa unawekeza moja kwa moja unakua unabadilisha maisha ya watu.
Lengo kuu la App hii ni kuhakikisha kuwa mamilioni ya watoto wanaweza kupata elimu kwa kupitia App hii katika pande zote za dunia.
Kumbuka pia O’Neal pia amewekeza katika makampuni makubwa kama vile Google, Apple na hata Ring (yametajwa machache tuu) hii inamaanisha kwamba sio mgeni katika sekta ya uwekezaji
Kingine O’Neal ameweka wazi kwamba sio mara zote amakua akiwekeza na kupata matokeo mazuri ila cha msingi ni kupanga mpango mkakati kabla ya kufanya hivyo.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment je unaonaje mienendo ya mwana kikapu huyu wa zamani katika uwekezaji?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.