Simu janja kutoka kwa Samsung bado zinaendelea kutoka moja baada ya nyingine na Galaxy S21 FE ipo katika mkao wa kula kuweza kultwa kwa wateja waliopo duniani kote.
Mambo yalivyo siku hizi si kitu cha ajabu kabisa kuona kampuni ya simu ikitoa simu janja hata tano kutoka familia moja na hivyo ndivyo ilivyo kwa Samsung ambao wapo njiani kutoa ndugu yake Galaxy S21. Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika baadhi ya sifa ambazo Samsung Galaxy S21 FE inazo ni:
Muonekano|Kipuri mama
Hapa simu hii inaelezwa kuwa na kioo chenye urefu wa inchi 6.4 ambacho ni kikuwa kuliko S21 (6.2) lakini kidogo kuliko S20 FE (6.5). Kwa upande wa kipuri mama zile ambazo zitakuwa ni kwa ajili ya soko la Ulaya na Amerika Kaskazini zitatuwa na mojawapo ya toleo la Exynos, za Korea Kusini zitawekwa Snapdragon 888.
Kamera|Betri
Hapa Samsung wameweka kamera ambazo zinavutia kwa kiasi chake hasa kwani inaonyesha upande wa nyuma simu hii ina MP 32, MP 12 na MP 8. Kwenye upande wa mbele inaonekana kuwa MP 12 tofauti na MP 32 iliyopo kwenye S20 FE.
Memori
Taarifa zinasema simu hii ina GB 8 za RAM, diski uhifadhi ni GB 128 au 256 lakini pia inaonekana kuwa na sehemu ya kuweka memori ya ziada. Mbali na hilo kuna uwezo wa toleo lenye RAM GB 6 kutoka pia kulingana na soko la wapi ambapo zitapelekwa.
One Comment