Samsung wamefanya tukio lao la kutambulisha Simu za Samsung Galaxy Z Fold, Z Flip 5, matoleo ya tableti ya Tab S9 na saa za Watch 6. Tukio hilo la kila mwaka linaloenda kwa jina la Unpacked, lilifanyika Julai 26 nchini Korea Kusini.
Tunakupa hapa sifa mbalimbali ya vyote vilivyotambulishwa katika siku hiyo.
Tukio hili lilitawaliwa zaidi na simu zao za mkunjo (fold).
Samsung Galaxy Z Fold 5
Simu ya Galaxy Z Fold 5 ndio toleo jipya la simu za mkunjo kutoka Samsung. Simu hii imekuja na maboresho kadhaa ukilinganisha na toleo la nyuma, kumbuka kama tulivyozungumza kwenye podcast yetu, bado simu za mkunjo zinapitia maboresho ya kiteknolojia ili kuwa nzuri zaidi. Katika Galaxy Z Fold 5 inaonekana Samsung ameboresha makosa mengi yaliyokuwa kwenye toleo lililopita.
- Display / Skrini – inchi 7.6
- Prosesa ya Snapdragon 8 Gen 2
- Teknolojia ya panapokunjika imeboreshwa zaidi.
- Flex mode: Hii inaipa simu yako uwezo wa kutumika kama laptop, eneo la nusu kuwa kama keyboard wakati nusu nyingine ikiwa ya kawaida.
Samsung Galaxy Z Flip 5
Kama kuna simu ambayo inaweza kukuvutia kuanza kutumia simu za mkunjo basi ni hii. Kwanza Samsung wamehakikisha inapatikana kwa bei ambayo haitishi sana, wakati inakuja na prosesa ile ile ya Galaxy Z Fold 5.
- Display / Skrini – inchi 6.7
- Prosesa ya Snapdragon 8 Gen 2
- Teknolojia ya panapokunjika imeboreshwa zaidi.
- Flex mode: Uchukuaji wa picha za selfie ni bora zaidi katika simu ya Galaxy Flip. Inakupa uhuru mkubwa zaidi kwani utaweza kutumia kamera zake kuu, na huku ukijiona kwenye kioo cha ziada, kile cha nyuma cha ukubwa wa inchi
Tableti za S9 Series
Kwenye tableti Samsung wanaleta tableti za aina 3 katika familia ya S9 Series, hizi ni Tab S9, Tab S9+ pamoja na Tab S9 Ultra.
- Display – Tab S9 inakuja na inchi 11, Tab S9+ inakuja na inchi 12.4, wakati Tab S9 Ultra ni ya inchi 14.6
- Prosesa ya Snapdragon 8 Gen 2
- Zote zinatumia kalamu janja: S Pen
Watch 6
Toleo jipya la saa janja ya Watch 6 limekuja na maboresho makubwa katika ubunifu wake kimuonekano na kiteknolojia. Kwa sasa wamewekeza zaidi katika teknolojia za upimaji wa masuala mbalimbali ya kiafya, pia prosesa ya haraka zaidi na betri linalodumu muda mrefu kuliko tulio lililopita.
Kwenye afya imejumuhisha uwezo wa kupima kiwango cha oksijeni kwenye damu.
Kwa ufupi:
Kifaa | Display | Prosesa | RAM | Storage |
Galaxy Z Fold 5 | 6.2-inch cover display, 7.6-inch main display | Snapdragon 8 Gen 2 | 12GB |
256GB, 512GB, or 1TB
|
Galaxy Z Flip 5 | 6.7-inch main display | Snapdragon 8 Gen 2 | 8GB | 128GB or 256GB |
Tab S9 | 11-inch display | Snapdragon 8 Gen 2 | 8GB | 128GB or 256GB |
Tab S9+ | 12.4-inch display | Snapdragon 8 Gen 2 | 8GB or 12GB | 128GB or 256GB |
Watch 6 | 1.4-inch display | Exynos W920 | 1GB | 16GB |
Bei
Hizi ni bei kulingana na bei zilizotangazwa na Samsung, kumbuka hadi zifike nchini bei inaweza kuongezeka kutokana na kodi na gharama zingine za kibiashara.
Kifaa | Bei ya USD | Makadirio(Tsh) |
Galaxy Z Fold 5 | Kuanzia $1,799 | 4,396,450 |
Galaxy Z Flip 5 | Kuanzia $999 | 2,418,378 |
Tab S9 | Kuanzia $899 | 2,168,975 |
Tab S9+ | Kuanzia $1,099 | 2,743,875 |
Watch 6 | Kuanzia $349 | 846,925 |
Tunategemea makala imekusaidia kufahamu kwa uharaka sifa na uwezo wa vile vilivyotambulishwa kwenye tukio la Samsung Unpacked.
Kumbuka Teknokona inakuletea vipindi kwa njia ya sauti, maarufu kama Podcasts, usipitwe, Tembelea hapa kusikiliza.
Kumbuka kushare na wengine.
No Comment! Be the first one.