Je wewe utaweza kukaa siku 99 bila kuingia Facebook?
Siku chache zilizopita ilifahamika ya kuwa Facebook ilitumia vibaya data za watu walizonazo kwa matumizi ya utafiti wao, kwa ajili ya kuboresha mifumo yao bila idhini ya watu husika. Hii ilihusisha tabia za kila siku za watu zaidi ya laki 7 kupitia matumizi yao ya kila siku wakiwa Facebook. Mashirika na watu mbalimbali wamekemea kitendo hicho na Facebook wamejikuta kwenye wakati mbaya na vyombo vya sheria kwenye baadhi ya nchi. Na sasa watu wengi wanataka kufanya vitu kuonesha kukwazika huko-> 99 Days of Freedom!
99 Days of Freedom kwa kiswahili siku 30 za Uhuru ni kampeni iliyoanzishwa na kampuni iitwayo JUST ya huko Uholanzi, na nia yake ni kujaribu kuhamasisha watu wengi zaidi kutotumia Facebook kwa takribani siku 99 ili kutambua ya kuwa wanaweza wakawa na maisha bora zaidi bila ya kutumia Facebook. Hadi muda huu ninaoandika makala hii kuna watu 3,141 wameshajiunga – unaweza kutembelea mtandao wao hapa-> http://goo.gl/zNj5N2
Ukiwa umejiunga utaungana na wengine wote mara kadhaa mtandaoni kuelezea hali yako kadri siku zinavyokwenda. Je wewe unaweza kuthubutu? Je unadhani inawezekana kuishi bila kutumia Facebook kwako kwa sasa? 🙂
Kumbuka kusambaza ujumbe huu kwa wengine, na tafadhali tuambie maoni yako hapa chini. 🙂
No Comment! Be the first one.