Ulishawahi kufikiria safari ya siku tano angani bila kubadilisha ndege? Sasa basi tumefika kwenye ulimwengu wa usafiri wa anga ambao hutahitaji kuunganisha ndege ili kufika unapokwenda.
Mamlaka ya usafiri wa anga ya Uingereza – CAA imetoa kibali kwa kampuni ijulikanayo kama Hybrid Air Vehicles (HAV) yenye makao yake katika mji wa Bedford kutengeneza ndege kubwa zenye uwezo wa kusafiri kwa muda mrefu (siku tano) bila ya kutua ardhini.
Kampuni inayotaka kuunda ndege ndefu zaidi duniani imepewa kibali na sasa iko mbioni kuunda ndege hiyo ianze kubeba abiria. Hatua hiyo inafuatia kufanikiwa kwa majaribio ya ndege ya mfano iliyopewa jina Airlander 10 ambapo mwaka 2016 ndege moja ilidondoka baada ya kuruka kwa dakika 30 ilipokuwa kwenye majarbio.
