Wiki iliyopita tuliangalia namba 20 hadi 11 katika simu zinazoshikilia chati kimauzo duniani na leo tunaangalia namba kumi hadi moja, kwa kujikumbusha zilizoshika namba 20 hadi 11 unaweza BOFYA HAPA! Nokia iliingiza simu nne katika chati hiyo wakati Apple waliingiza iPhone tatu huku Motorola iliingiza simu mbili na Samsung iliingiza simu moja, je mambo yatabadilika katika 10 za juu? Endelea kusoma;
Nafasi ya 10 inashikiliwa na Nokia 3310 (3330) iliyotoka mwaka 2000 na simu hii iliuzika kwa zaidi ya nakala milioni 126. Hii bila ubishi wengi mtakuwa mnaikumbuka kwani hata nchini kwetu ilionekana karibia kwa kila mwenye simu enzi nzileeee 🙂
Namba 10: Nokia 3310
Ilitolewa Mwaka: 2000
Idadi ya Mauzo: Milioni 126
Nokia 1600 (1650/1661) iliyoingia sokoni mwaka 2006 inashikilia namba tisa kimauzo kwa kuuza takribani nakala milioni 130
Namba 9: Nokia 1600
Ilitolewa Mwaka: 2006
Idadi ya Mauzo: Milioni 130
Namba nane inashikiliwa na simu iliyouzika kuliko zote kutoka kwa Motorola, na hii ni Motorola RAZR V3 iliyotoka mwaka 2004.
Namba 8: Motorola RAZR V3
Ilitolewa Mwaka: 2004
Idadi ya Mauzo: Milioni 130
Simu nyingine kutoka Nokia inashikilia namba 7, na hii ni Nokia 2600 (2610/2626/2630) ya mwaka 2004..
Namba 7: Nokia 2600
Ilitolewa Mwaka: 2004
Idadi ya Mauzo: Milioni 135
Je unafikiri simu iliyouzika kuliko zote kutoka Samsung ni ya toleo la Galaxy? Hapana, ni Samsung E1100 iliyoingia sokoni mwaka 2009 na inashika nafasi ya 6 na siyo ya Android.
Namba 6: Samsung E1100
Ilitolewa Mwaka: 2009-2012
Idadi ya Mauzo: Milioni 150
Nafasi ya tano inaenda kwa Nokia 6600 iliyotoka mwaka 2003 na ilifanikiwa kuuza nakala milioni 150. Simu hii iliyokuwa inatumia programu ya uendeshaji ya Symbian ilikuwa moja ya simu ghari zaidi ilipotoka, ilikuwa inauzwa kwa zaidi ya milioni 1.2 za kitanzania.
Namba 5: Nokia 6600
Ilitolewa Mwaka: 2003
Idadi ya Mauzo: Milioni 150*
Nokia 5230 inashikilia nafasi ya nne kwa mauzo ya zaidi ya nakala milioni 150, simu hii ilitoka mwaka 2009
Namba 4: Nokia 5230
Ilitolewa Mwaka: 2009
Idadi ya Mauzo: Milioni 150*
Nokia 1200 iliyoingia sokoni mwaka 2007 inashikilia nafasi ya tatu kwa mauzo ya zaidi ya nakala 150. Je ulishawahi kutumia simu hii? Nakumbuka tatizo lake kubwa lilikuwa ni kuvimba kwa kipadi zake baada ya matumizi ya muda mrefu.
Namba 3: Nokia 1200
Ilitolewa Mwaka: 2007
Idadi ya Mauzo: Milioni 150*
Nafasi ya pili inakwenda kwa Nokia 3210 iliyoingia sokoni mwaka 1999 iliyofanikiwa kuuzika kwa zaidi ya nakala milioni 160.
Namba 2: Nokia 3210
Ilitolewa Mwaka: 1999
Idadi ya Mauzo: Milioni 160*
Nafasi ya kwanza inashikiliwa na simu mbili, zote kutoka Nokia. Hii ni kwa sababu taarifa zao za kimauzo zinautofauti utofauti kidogo na hivyo mara nyingi inakuwa ni bora kuziweka katika sehemu moja. Na hizi ni Nokia 1100 ya mwaka 2003 pamoja na Nokia 1110 ya mwaka 2005 na kila moja imeuza zaidi ya nakala milioni 250, hivyo kwa ujumla wake kuna zaidi ya nakala milioni 500.
Simu yangu ya kwanzu kutumia ipo katika orodha hii, wewe je? Na umegundua jambo moja katika orodha hii? – Nokia ndiye mwenye simu nyingi zaidi.
No Comment! Be the first one.