Mwaka ndio unaishia, lakini ni simu ipi bora kwako? Ukiachana na upendeleo au hata ushabiki wa simu fulani kuna maeneo mengi ya kuangalia katika kubaini kama simu ni bora au si bora. Kwa mfano unaweza tazama katika uwezo wa kamera na maeneo mengine mengi kama vile kuendana kwa bei na sifa.Teknolojia inavyozidi kukuwa inasababisha mapinduzi ya hali ya juu, kumbuka simu janja zote zinategemea teknolojia hii. Ili ziingie sokoni na zifanye vizuri inabidi zitumie teknolojia ya hali ya juu ili kuleta mambo mapya. Miaka kumi iliyopita wakati unacheza mchezo (game) la nyoka katika simu (kisimu) chako cha nokia tena chenye kioo cha rangi moja (wino mweusi) ulitegemea kama utakuja kucheza michezo kama candy crush au hata temple run? Usinijibu..
Sasa utagunduaje simu bora? hapa ndipo wataalamu wanapokaa chini na kuanza kuzichabua simu janja na kuja na jibu kuwa zipi ni bora kabisa
Tuzifahamu Simu janja Bora Kwa Mwaka 2015
- Simu Janja Bora Ya Android: Samsung Galaxy Note 5
Simu janja hii kutoka samsung ni ya aina yako na iko mstari wa mbele ukilinganisha zingine za Andriod. Simu hii ina kioo cha nchi 5.7 na ina umbile la kuvutia kabisa. Pia inaweza ikawa ndio simu yenye kamera nzuri kwa sasa kutoka android (MP 16). Katika soko la leo simu hii ni rahisi sana kuwa namba moja kwa zile zinazotumia programu-endeshaji ya Android.
- Simu Janja Bora Ya iOs: Apple iPhone 6s
Kwa simu janja ambayo imeongoza kuja na ubunifu mwaka huu ni iPhone 6. Hii imepelekea mpaka simu hiyo kuwa na mauzo ya juu kabisa zaidi ya simu zingine nyingi kwa mwaka huu. Fikiria kitu kama “Tachi ya 3D” kilivyobadilisha jinsi tunavyoweza tumia simu zetu.
Soma Uchmbuzi Wetu mfupi Juu Ya Simu Hii Hapa
- Simu Janja Bora Yenye Thamani Ndogo: Motorola Moto G (2nd Gen.)
Hii inatoka katika kampuni la motorola. Unapokuwa unajaribu kutafuta simu ya kununua tena ya bei ya kawaida inakubidi uwe makini. Kuna simu nyingine sawa ni bei rahisi lakini zinajiwekea mambo makubwa na mazito ambazo haziwezi kuhimili (mfano simu nyingi za kichina). Ukinunua Moto G, itakuwa imeenda sambamba na pesa zako, sawa! itakubidi uvumilie kamera yake huku ukifurahishwa na vitu vingine kama uwezo wake wa kukaa na chaji.
- Simu Janja Yenye Kamera Bora: Samsung Galaxy Note 5
Kipengele cha kamera katika watengenezaji wa simu wengi wa mwaka 2015 wamekiboresha. Baada ya makampuni hayo kuweka mezani nini kipya katika kamera za simu zao, samsung Note 5 inaibuka kidedea. Kama nlivyosema awali simu ni ya megapixel 16 kwa kamera ya nyuma na MP 5 kwa kamera ya mbele. Kama wewe ni mpenzi wa picha utaungana nami kuwa simu hii ni bora katika sekta hii ya picha.
Siku hizi karibia kila mtu anamiliki simu janja. simu hizi ni vifaa ambazo vinatusaidia katika kuungna na watu katika mawasiliano kwa ujumla. Na ili simu hizo ziwe na hadhi ya kipekee kwa soko hili la leo ni lazima makampuni yake yafanye kazi ya ziada.
No Comment! Be the first one.