Je unatumia simu ya android ambayo imekuwa slow sana kiasi kwamba inakukwamisha kuifurahia? makala hii itakupatia baadhi ya njia ambazo zitakusaidia kuiongezea kasi simu yako na kuirudisha katika hali yake iliyokuwanayo ulipoanza kuitumia.
Zipo sababu nyingi ambazo zinaweza kuifanya simu yako ya android iwe slow, nitakupa sababu moja moja na kisha njia ya kuweza kuchukua ili kuiondoa hali hiyo kulingana na sababu hiyo.
-
Kuzima app ambazo hauzitumiii na zinajiendesha katika background.
Simu janja zote zina uwezo wa kuendesha app katika background, iwapo haujazisimamisha app hizi ama haujaizima simu yako hata kwa wiki basi app ambazo zinafanya kazi katika background zitaendelea na kuifanya simu yako kuwa slow. Hapa unachotakiwa ni kuzima app zote ambazo unajua hauzihitaji kuendelea kufanyakazi katika background.
-
Un-install app zote ambazo hauzitumiii ama ambazo hautegemei kuzitumia hivi karibuni.
Ni kawaida kwa watumiaji wengi wa Simu janja kujikusanyia app nyingi katika simu hata zile ambazo hawana matumizi nazo, hii inafanya kwamba simu zetu kuwa na mzigo mzito ambao hauna manufaaa. App zinavoongezeka katika simu hupunguza kasi ya simu kufanya baadhi ya mambo hivyo inashauliwa kwamba kila wakati mtumiaji wa simu anadelete app ambazo hazina umuhimu.
-
Kuondoa widget zote ambazo hauzitumii.
Widget ambazo mara nyingi tunazikuta pindi tunaponunua simu zetu zikiwa zimewekwa katika ukurasa wa mwazo wa skriini ni moja ya chanzo cha kufanya simu zetu kuwa slow maana zinachukua nafasi kubwa na nguvu kubwa ya simu ambayo ingeweza kutumiwa na simu kuongeza kasi katika utendaji wake wa kila siku. Kulitatua hili ni kuhakisha kwamba unafuta widget zotea ambazo huwa zinakuwa katika skrini ya mwanzo ya simu na unaziacha zile tu ambazo ni za muhimu kwako.
-
Ku-update software ya simu yako.
Simu ambayo haina software ambayo ni ya karibuni zaidi maranyingi inashindwa kufanya kazi katika kiwango na kasi inayotakiwa hivyo ni busara kuhakikisha kila wakati software ya simu yako inaenda na wakati kwa kuwa na software ambayo ni toleo la karibuni kabisa. Kuangalia kama simu yako inaendeshwa na software ambayo inaenda na wakati fungua Settings>about phone> systems update. kama kunatoleo jipya zaidi la software basi hapa litaonekana nautalipakua na kuanza kulitumia.
-
Kui-Reset simu yako irudi katika hali ya kiwandani.
Hii njia huifanya simu kurudi katika hali yake ya upya wa kiwandani, njia hii itafuta vitu vyote ambavyo uliviweka katika simu hivyo ni muhimu kuhakikisha kwamba umekwisha hifadhi data na taarifa zako muhimu.
Zipo njia nyingine mbali mbali kwaajiri ya kufanya simu yako iweze kurudia spidi yake yake ya awali lakini hizi tano nilizo zitaja ndio zenye nguvu zaidi. Ukiisha zifuata hizi na kuona bado simu yako ipo slow basi tafuta msaada wa mtu ambaye anaujuzi ama ufundi wa simu.
One Comment
Comments are closed.