Pamoja na mfumuko wa simu nyingi zisizo za kiwango cha kimataifa hasa zinazotengenezwa China, lakini kuna simu zinazozalishwa nchini humo ambazo hujawahi kuzisikia lakini zina ubora juu na kushindana na za makampuni makubwa kama Samsung na wengine.
Kwa mazoea yetu unapozungumzia kununua bidhaa kutoka nchi ya China hususani simu janja(Smartphone) wengi hutazama ni kama kununua au kukabiliana na Busu la kifo.
Simu janja za China zimekuwa zikishambuliwa kwa madai mengi yakiwemo kwamba ni Feki, ubora mdogo na hazina Warrant wa kuaminika.
Kama ulikuwa unafikiri hakuna simu bora zinazozalishwa China basi umekosea. Tutakuwekea hapa simu saba zinazotengenezwa China ambazo zina kiwango bora kuanzia Prosesa, RAM mpaka muonekano wake.
Anza kupitia moja baada ya nyingine na ukitaka sifa za simu hizo kwa ukamilifu wa kila kilichomo waweza kupitia mtandao wa www.gsmarena.com.
ZUK Z2 PRO

Hii ni Simu Janja ambayo si kwa ajili ya matumizi ya Facebook tu, Z2 ina uwezo mzuri kufanya mambo mengi zaidi.
Sifa zake:
- Prosesa ya Snapdragon 820,
- Ukubwa wa RAM ni 6GB
- Ukubwa wa kioo ni nchi 5.2, (1080p AMOLED)
- Uwezo wa kuhifadhi data ni 128GB
- Kamera yenye Megapixel 13 (autofocus and dual-LED flash)
- Betri ya uwezo wa 3100 mAh
Simu hii ilizinduliwa April 2016 na kuanza kuuzwa Juni 2016. Bei yake ni Dola 276 (Takribani Tsh 612,940/=)
LEECO LE MAX 2

LeEco wachina halisi, hawa wanafahamika kama watengenezaji wa magari ya umeme, TV nk. Lakini katika ulimwengu wa Simu Janja hawapo nyuma. Simu hii ni ya kiwango cha juu kuanzia cover lake, kamera mpaka prosesa.
Simu janja hii itakufanya uisahau Samsung Galaxy Note 7 iliyositishwa na kampuni ya Samsung kwa matatizo ya kulipuka kwa betri zake.
Sifa zake ni hizi.
- Prosesa ya snapdragon 820
- Ukubwa wa ram ni 6GB
- Ukubwa wa kioo ni nchi 5.2, (1440×2560 IPS LCD)
- Uwezo wa kuhifadhi data ni 128GB
- Kamera yenye megapixel 21
- Betri ya uwezo wa 3100 mAh
Simu hii ilizinduliwa April 2016 na kuanza kuuzwa Mei 2016. Bei yake ni dola 185 (yenye uhifadhi data 32GB), (Takribani Tsh 410,800/=)
VIVO XPLAY 5 ELITE

Wakati ilipotangazwa kuzinduliwa Simu Janja hii mwezi machi 2016, iliwashangaza wengi
kwa kuwa na sifa zinazofanana sana na simu za Samsung note 7 na Samsung S7. Tofauti kubwa ni
jina na logo.
Sifa zake ni hizi.
- Prosesa ya Snapdragon 820
- Ukubwa wa ram ni 6GB
- Ukubwa wa kioo ni nchi 5.4, (1440×2560 CURVED AMOLED)
- Uwezo wa kuhifadhi data ni 128GB
- Kamera yenye megapixel 16
- Betri ya uwezo wa 3100 mAh
Simu hii ilizinduliwa na kuuzwa Machi 2016. Bei yake ni dola 669 (Takribani Tsh 1,500,000/=).
COOLPAD COOL S1

Kesi nyingine hii. Ni kama uigaji fulani hivi. Simu hii imefanana sana na simu ya One Plus 3T.
Karibu kila kitu kinaendana, ikiwa pamoja na Prosesa, ukubwa wa uhifadhi wa data. Japo upande wa kioo wametumia cha IPS badala ya Amoeled.
Sifa zake ni hizi.
- Prosesa ya snapdragon 821
- Ukubwa wa ram ni 6gb
- Ukubwa wa kioo ni nchi 5.5, (1080p IPS LCD)
- Uwezo wa kuhifadhi data ni 128GB
- Kamera yenye megapixel 16
- betri ya uwezo wa 4070 mAh
Simu hii ilizinduliwa Desemba 2016 na kuanza kuuzwa januari 2017. Bei yake ni dola 280 (Takribani Tsh 621,000/=)
ULEFONE GEMINI PRO

Simu hii ilitangazwa mapema mwaka huu lakini sio katika mkutano wa Mobile World Congress(MWC). Unataka kujua muonekano wa simu hii? Ina muonekano kama iPhone 7 Plus. Ina kamera mbili. Bei yake ipo poa sana na ni ni simu bora.
Sifa zake ni hizi.
- Prosesa ya Mediatek Helio x27
- Ukubwa wa Ram ni 4GB
- Ukubwa wa kioo ni nchi 5.5, (1080p IPS LCD)
- Uwezo wa kuhifadhi Data ni 128GB
- Kamera yenye Megapixel 13
- Betri ya uwezo wa 3250 mAh
Imeanza kuuzwa mapema mwaka huu. Bei yake ni dola 139 mpka 190 (Takribani Tsh 310,000/= – Tsh 420,000/=).
GIONEE A1 PLUS
Kwa wale wapenzi wa kujipiga Selfie, kwa simu hii ndio utapenda zaidi. Ina kamera nzuri na yenye uwezo mkubwa.
Sifa zake ni hizi.
- Prosesa ya Mediatek Helio P10
- Ukubwa wa Ram ni 4GB
- Ukubwa wa kioo ni nchi 6, (1080p IPS LCD)
- Uwezo wa kuhifadhi Data ni 64GB
- Kamera yenye Megapixel 13 (20MP kwa kamera ya mbele kwa ajili ya selfie)
- Betri ya uwezo wa 4000 mAh
Simu hii imezinduliwa Februari 2017 na inatarajiwa kuuzwa April mwaka 2017
MEIZU PRO 6
Hii ni moja simu Janja bora kutoka China. Sifa na uwezo wake inaweza kupambana na simu zinazozalishwa na Iphone pamoja Samsung. Simu hii inatumia prosesa bora na nzuri kwa sasa ya ya Exynos 8890. Ni simu ya kifahari ambayo usingependa kuikosa. Uzuri utaipata kwe bei ndogo.
Sifa zake ni hizi.
- Prosesa ya Exynos 8890
- Ukubwa wa RAM ni 4GB
- Ukubwa wa kioo ni nchi 5.2, (1080p amoled)
- Uwezo wa kuhifadhi data ni 128GB
- Kamera yenye Megapixel 21
- Betri ya uwezo wa 2560 mAh
Simu hii ilizinduliwa april 2016 na kuanza kuuzwa Mei 2017. Bei yake ni Dola 287 (Takribani Tsh 638,000/=).