Kama utakua umeshagundua siku hizi simu janja nyingi sana betri zake huwa ni za moja kwa moja kwa maana ya kwamba haziwezi kutolea bila kuzipeleka kwa mtaalam
Sasa tunajiuliza mbona zamani tulikua tunaweza kutoa betri za simu zetu wenyewe? yaani ilikua ni rahisi kiasi cha kwamba hata kama betri muda wake wa matumizi umeisha …..
…bado tulikuwa na uwezo wa kuwenda kununa betri jipya na tukafungua mfuniko wa simu na tukabadilisha betri hilo wenyewe? Hapa inabidi tujiulize kwanini simu janja za siku hizi betri zake hazitoki.
Sababu za haraka haraka ni kama;
- Betri ya simu imewekwa ndani ili kuhakikisha simu inakua na umbo dogo zaidi
- Betri imefungiwa ndani ili kuhakikisha kuwa simu zinakuwa na uwezo wa kuzuia kuingia maji.. kipengele hichi ni kizuri sana maana warranty nyingi za simu huwa hazipokei kurekebisha simu iliyoharibika kwa kuingia maji.
- Kingine ni kwamba betri za moja kwa moja zinaweza kukusaidia kujua simu yako ilipo kama utakua umeibiwa kwa uharaka zaidi na ndani ya muda mchache kama utaweza kuwahi maana mtu alieiba atakuwa hajaizima hivyo unaweza tumia teknolojia zile kama za find my phone.. kutafuta kifaa chako
- N.k
Hali ya kuwa na betri la moja kwa moja kwa muuzaji lina kafaida kidogo, hebu fikiri ukiwa na simu ambayo betri lake halitoki. Hii inamaana kwamba utakuwa unatumia simu yako..
….Betri litaanza kuchoka na kisha utakua unachaji simu yako mara kwa mara mpaka utaanza kufikiria kununua simu mpya.. kwa wauzaji wa simu hapo ni kama wamecheza na akili zetu ili wazidi kuuza.
Ningependa kusikia kutoka kwako, je unadhani kuna sababu zingine ambazo naweza kuwa nimezisahau? naomba niandikie hapo chini katika eneo la comment.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Kila Siku Sababu Tuko Na Wewe Katika Teknolojia Kila Siku!.
No Comment! Be the first one.