Oppo ni kampuni kubwa sana ambayo inajihusisha na teknolojia nyingi ikiwemo kutengeneza na kuuza simu na sasa imekuja na toleo la Oppo Find N2.
Toleo hili ni toleo jipya na muendelezo wa matoleo ya Oppo Find N, lakini pia tuliandika kuhusu fununu kuhusiana na simu hii. Soma zaidi >>HAPA<<
Oppo Find N2 ni moja kati ya zile simu janja za kujikunja, na imeingia sokoni mahususi ili kuleta ushindani wa juu kwa wapinzani.
Kingine ni kwamba simu hii kutoka Oppo ndio simu janja ya kwanza kutoka china ambayo ni ya kujikunja na inapatikana nje ya china (soko nje ya china).
Kingine ni kwamba kampuni ya Oppo ni moja katika ya kampuni makubwa sana kutokea china na mpaka sasa katika rekodi za kidunia ni kampuni ya 4 katika watengenezaji na wauzaji simu wakubwa.
Oppo Find N2 Flip imezinduiwa rasmi jumatano, huku ikiwa na vioo viwili, kioo kikubwa kina ukubwa wa inchi 6.8 na kioo hiki kinaweza kuonekana kama simu ikifunguliwa.
Kioo kingine ni kile ambacho kinapatikana nje (wakati imejifunga) na oppo wenyewe wanajisifia kua na kioo kikubwa cha aina hiyo.
Oppo kupitia simu hiyo wamejisifia kwamba ina uwezo wa kufungua na kufunga mara 400,000 ambapo kwa haraka haraka ni kwamba kwa siku atafungua na kufunga mara 100 kwa kipindi cha miaka 10 (kwa hesabu ya makadirio).
Simu hii pia ndio simu ya mashindano ya ligi ya mabingwa ya ulaya (UEFA Champions League) na inafanya hivyo katika kuhakikisha kuwa inaendelea kijitangaza n.k.
Sifa Zake Za Undani
Kamera yake ya mbele (selfie) iko na 32MP, uwezo wake wa utambuzi wa alama za vidole (finger print) upo katika kitufe cha kuzima/kuloki simu.
Nyuma ina kamera mbili huku kamera kubwa ikiwa na 50MP huku ile nyingine ya kupiga eneo kubwa (ultra wide) ikiwa na 8MP.
Uwezo wa betri ni 4,300 mAh na inakua na uwezo wa fast charging (uwezo wa kuingiza chaji kwa haraka).
Hizi ni baadhi za sifa zake za undani, Soma kila kitu kuhusiana na Oppo >>HAPA<<
ningependa kusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini katika eneo la comment, je unadhani sifu hii itaweza kushindana na simu kutoka makampuni mengine kama Samsung, Apple n.k?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.