Oppo wametangaza ujio wa simu zao mpya za matoleo ya Oppo Find N ambapo toleo linakuja na simu janja za aina mbili.
Majina ya simu hizo kutoka Oppo ni Foldable Find N3 na Find N3 Flip ambazo zote zitakuja na muonekano na sifa za undani za aina yake.
Ni wazi kwa sasa masoko ya simu za kujikunja yanakua kadri siku zinavyozidi kwenda na simu za aina hii kutoka Oppo zinakua ni mshindani mkubwa katika soko.
Oppo wanajisifia kwani wanasema wanataka watu wapate thamani ya kompyuta katika mfuko wako.
Sifa Za OPPO Find N3 Ni Hizi Hapa
OPPO Find N3 inakuja na kioo kikubwa cha inchi 7.82 2K (2,268 x 2,440 pixels) LTPO 3.0 AMOLED.
Kioo cha nje ni 6.31-inch 2484 x 1116px AMOLED ambacho kinakuja na 10-120Hz refresh rate.
Simu hii inakuja na uwezo wa laini mbili zile ndogo kabisa (Nano) huku ikiwa inaendeshwa na mfumo wa Android 13.
Oppo Find N3 inakuja na chip ya Qualcomm’s octa-core Snapdragon 8 Gen 2 SoC huku ikiwa na Adreno 740 GPU, kuja na ukubwa hadi wa 16GB ya LPDDR5X RAM
Kwa upande wa kamera , OPPO Find N3 inakuja na kamera tatu ambapo moja ina 48-megapixel Sony LYTIA
Nyingine ikiwa na 64-megapixel OmniVision OV64B sensor huku ikiwa na uwezo wa 3x optical zoom,
Nyingine ina 48-megapixel ikiwa na sense ya Sony IMX581. Huku kamera ya selfi ikiwa na 20-megapixel huku ikiwa ndani ya kioo
Kwa upande wa kioo cha ndani pia kuna kamera ya selfi ambayo ina 32-megapixel
Vile vile ina kipengele cha utambuzi wa alama za vidole (finger print), uwezo wa kutoa loki na sura (face unlock) vile vile betri yake inakuja na uwezo wa 4,805mAh
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, je hii umeipokeaje na je ushawahi kutumia vifaa vya Oppo.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.