Google wapo mstari wa mbele kutoa masasisho ya programu endeshi kwenye simu/kompyuta na hivi karibuni wametoa programu endeshi waliyoiita “Andriod P”. Android P tayari ipo sokoni lakini sio simu zote zinazotumia Android zitaweza kupata sasisho hilo jipya.
Programu endeshi mpya inapotoka watumiaji wengi wa simu rununu wanapenda kujua iwapo sashisho jipya lililotoka lina kipi kipya na hii imekuwa ni kawaida kwa watumiaji wote wa Andoid na iOS ingawa hata kama sasiho jipya limetoka lakini ikatokea toleo la nyuma likatokea kupendwa zaidi.

Simu janja ambazo hazitopata sassiho la Android P mbali na Pixel C ni Nexus 5X, Nexus 6P na sababu iliyoelezwa Google kufanya hivyo ni kwa mwaka huu (2018) wameamua kuangalia zaidi simu ambazo zina miaka miwili sokoni; Nexus 5X, Nexus 6P na Pixel C zilitoka mwaka 2015 zikiwa na Android 6.0 Marshmallow. Hata hivyo, simu mu hizo zitaendelea kupata masasisho kwa ajili ya kuzifanya simu zao kuwa salama. Masasisho hayo yataenda mpaka mwezi Novemba 2018 na kama ni masasisho ya programu endeshi yatakomea Android 8.1.
Tukiangazia wapinzani wakubwa wa Google ambao ni Apple wao wenyewe wameruhusu simu rununu iPhone 5S, iPad mini 2 na hata kizazi cha 6 cha iPod ya mguso kuweza kupokea masasisho ya kuhamia iOS 11 ambalo ni toleo la hivi sasa la programu endeshi kutoka Apple.

Nexus Player ambayo ilitoka mwaka 2014 pia haikuorodheshwa kama itakuwa inapata masasiho yoyote kutoka Google. Je, wewe unatumia simu mojawapo zilizo orodheshwa kutopata sasiho la programu endeshi ya Android P? Tuandikie maoni yako hapo chini.
Vyanzo: Gadgets 360, The Verge
One Comment
Comments are closed.