Kampuni ya Apple imethibitisha kwamba simu yake mpya ya iPhone haitakuwa na tundu la kawaida la kifaa cha kusikiza sauti (Earphones), kwa Kiingereza hufahamika kama ‘audio jack’.
Simu hiyo ya iPhone 7 badala yake itatumia teknolojia ya Apple ya lightning ambayo itamuwezesha mtu kutumia tundu moja kuunganisha simu na vifaa vingine.
Apple pia watavumisha kutumiwa kwa visilikizia sauti ambavyo havitumii nyaya, na imetoa aina yake ya earphone zinazojulikana kama Airpods.
Sifa za Airpods
- Airpods ni visikilizia sauti vyenye ukubwa wa 3.5mm kilivumishwa sana na vicheza muziki vya Walkman vya kampuni ya Sony, lakini kilitumiwa mara ya kwanza katika redio zilizotengenezewa Japan mwaka 1964.
- Zina uwezo wa kugundua zinapoingizwa masikioni. Hii inaziwezesha kusitisha uchezaji muziki zinapochomolewa masikioni.
- Unaweza pia kuzielekeza kwa kutumia programu ya Siri. Hata hivyo, lazima ziwekwe chaji kivyake ingawa Apple inasema zinaweza kukaa na chaji kwa hadi saa tano. Kifaa chake cha kuhifadhia kinawezesha mtu kutumia kwa hadi saa 24.
Kampuni hiyo imesema imehitaji kutumia ujasiri kuchukua hatua hiyo. Hata hivyo, hatua hiyo huenda ikawaudhi baadhi ya wateja ambao sasa watahitajika kununua kifaa unganishi yaani adapter ndipo waweze kutumia visikilizia sauti.
Apple wamezindua iPhone 7 baada ya kipindi cha mwaka mmoja cha kushuka kwa mauzo ya simu za iPhone na kupungua kwa sehemu inayodhibitiwa na kampuni hiyo sokoni.
Sifa nyingine za iPhone 7
- Kitufe cha nyumbani sasa kinaweza kutofautisha uzito kinapobonyezwa na kutoa mtikisiko. Kitufo hicho sasa hakiingii ndani ya simu.
- Simu hizo zinaweza kuingizwa ndani ya maji ya kina cha 1m (3.2ft) kwa dakika 30 wakati mmoja bila kuharibika
Aina kubwa ya iPhone 7 Plus ina lensi mbili za kamera sehemu ya nyuma, ambayo inaimarisha uwezo wa kupiga picha.
Bei ya iPhone 7
£599 hadi £799 ($799-$1,066)|Tsh 1,745,815-Tsh 2,329,210, kwa kutegemea uwezo wake wa kuhifadhi data. Kwa iPhone 7 Plus ni kuanzia £719 hadi £919 ($959-$1,226)|Tsh 2,095,415-Tsh 2,678,810.
Hiyo ndiyo iPhone 7 iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na wengi. TeknoKona imekuhabarisha kama kawaida yake.
Vyanzo: BBC, the guardian
2 Comments
Comments are closed.