Kampuni ya Apple jana Jumatano usiku kwa saa za Afrika Mashariki imezindua simu zake mpya tatu za iPhone kwa mwaka 2018 ambazo ni iPhone XS, iPhone XS Max na iPhone XR lakini bila kusahau Apple Watch 4.
Uzinduzi huo umekuja baada ya tetesi nyingi kuzagaa kwa miezi kadhaa kuhusu ujio wa simu hizo ambapo waandishi wa masuala ya kiteknolojia hususani simu wamekuwa wakitoa taarifa mbalimbali kuhusu ujio wa matoleo hayo ya simu za iPhone.
Muonekano wa simu hizi mpya ni kama ule wa iPhone X iliyotoka mwaka jana na inaelezwa kuanzia sasa muonekano kwa simu za iPhone zitakuwa zikifanana na iPhone X.
Matoleo haya yanafanya mapinduzi makubwa kwa simu za iPhone kwa kuwa na aina ya kioo kikubwa tofauti na matoleo ya kipindi cha nyuma.
Tuangalie kwa ufupi undani wa simu hizo za lakini tambua kwamba tofauti kati ya iPhone XS Max na iPhone XS ni ukubwa wa kioo tu.

Wasifu wa iPhone XS Max.
Mawasiliano: 2G, 3G, 4G
Kioo: Super AMOLED, ukubwa wa inchi 6.5
Mfumo endeshi: iOS 12
Uwezo na aina ya Prosesa: Hexa-core, Apple A12 Bionic
Ukubwa wa ndani: 64/256/512 GB
Ukubwa wa RAM: 4GB
Kamera ya nyuma: Zipo mbili, moja ina 12 MP, f/1.8, 28mm, 1.4µm, OIS, PDAF na nyingine ina 12 MP, f/2.4, 52mm, 1.0µm, OIS, PDAF, 2x optical zoom.
Kamera ya mbele: 7 MP, f/2.2, 32mm
Aina ya Betri: Li-ion
Ukubwa wa Betri: Bado haijawekwa wazi ukubwa wake
Bei: 1,250 EUR (Tsh. 3,300,000/-)
Rangi: Kahawia, Fedha, Dhahabu

Wasifu wa iPhone XR
Mawasiliano: 2G, 3G, 4G
Kioo: IPS LCD , ukubwa wa inchi 6.1
Mfumo endeshi: iOS 12
Uwezo na aina ya Prosesa: Hexa-core, Apple A12 Bionic
Ukubwa wa ndani: 64/128/256GB
Ukubwa wa RAM: 3GB
Kamera ya nyuma: 12 MP, f/1.8, 28mm, 1.4µm, OIS, PDAF
Kamera ya Mbele: 7 MP, f/2.2,
Aina ya Betri: Li-ion
Ukubwa wa Betri: Bado haijawekwa wazi ukubwa wake
Bei: 850 EUR (Tsh. 2,255,000/-)
Rangi: Nyeusi, Nyekundu, Njano, Bluu.
