Watengenezaji wa vifaa vya mawasiliano wanazidi kufanikiwa katika kupunguza unene/ukubwa wa vifaa kama simu kompyuta mpakato (laptop) na tablet. Imekuwa ni ndoto ya siku nyingi kutengeneza simu kompyuta mpakato (laptop) na tablet nyembamba na ambazo zinaweza kutunza umeme kwa muda mrefu zaidi.
Kampuni ya Intel ambayo ni watengenezaji wa kubwa wa chip zinazo tumika katika simu tablet na hata kompyuta wamefanikiwa kutengeneza chip ndogo zaidi hivi karibuni. Intel 14nm ‘Broadwell’ Wafer maarufu kama Core M processor kutoka kwa kampuni hiyo ya intel ni processor ambayo itatumia transistor zenye ukubwa wa 14nm (chip nyingi za sasa zinatumia transistor zenye 22nm).
Processor hiyo ya intel ya Core M itapunguza matumizi ya umeme kwa asilimia 60 (maana yake ni kwamba betri ya kifaa itatumika kwa kiasi kidogo zaidi) na pia itakua ni nusu ya processor ya zamani kwa ukubwa (hii maana yake ni kwamba ukubwa utashuka kwa asilimia 50 kwa vifaa).
Ijulikane kwamba bado yapo majaribio na majadiliano yenye malengo ya kupunguza saizi ya processor kwa kutengeneza chip zilizo katika saizi ya 10nm, hii ni kusema kwamba bado tunayo nafasi ya kuona kompyuta na tablet nyembamba zaidi ya Lenovo ThinkPad Helix na the HP Envy X2
No Comment! Be the first one.