Oppo ni chapa kubwa sana ya kutengeneza na kuuza simu, ni moja kati ya washindani wazuri sana katika soko la simu janja. Mara nyingi kampuni hii iko katika kumi bora ya uuzaji wa simu janja.
Kwa mwaka jana ilikuja na simu ya kujikunja (fold) na simu hiyo –Oppo Find N– iliingia sokoni na kuanza kuchuana na matoleo ya Galaxy Fold na Mix Fold kwa sasa iko katika hatua za mwanzo kabisa za kuja na simu janja ya kujipindua (flip).
Ni wazi kuwa simu janja za kujikunja (fold) ziko tangia zamani (teknolojia hii sio mpya) ukilinganisha na teknolojia ya kujipindua (flip).
Kwa taarifa zilizopo ni kwamba inategemewa simu jaja hiyo kuja na vioo viwili huku kioo cha uso wa nje kikiwa na ukubwa wa inchi 3.26 na ule ukubwa wa ndani ikiwa ni inchi 6.8.
Vioo hivyo vyote viwili vitakua na mfumo wa OLED huku ujazo wa betri lake ukiwa ni 4.300mAh.
Katika upande wa kamera na kwenyewe ni kwamba kamera ya selfi itakua na 32MP, Kamera yake kuu ikiwa na uwezo wa 50MP, kamera ambayo itatumika kipiga picha eneo kubwa (ultra-wide) ikiwa ni 8MP huku sensa za kamera hizo zikiwa zinatoka katika kampuni ya Sony.
Mpaka sasa ni bado taarifa hizi hazijathibitishwa lakini kutokana na vyanzo mbalimbali vilivyoleta hizi taarifa vinaaminika ni kwamba kuna hati hati kubwa ikawa ni taarifa za kweli.
Chanzo: GSMArena
Ningependa kusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini katika eneo la comment, je unadhani kwa baadhi ya sifa tajwa hapo juu simu janja hii itaweza kuleta ushindani wa hali ya juu kwa simu nyingine katika soko?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.