Ni wazi kuna simu zenye RAM zenye GB kubwa lakini hatujawahi kuona ile ambayo inafika mpaka 24GB sio? Hakika hii ndio ya kwanza.
Simu hii inaitwa RedMagic 8S Pro na imezinduliwa huko nchini China, japo kwa sasa inapatikana tuu katika soko hilo.
Lakini kwa jinsi hali inavyozidi kwenda itaanza kupatikana kwa masoko ya dunia nzima hivi karibuni maana ni simu shindani kabisa na hizi ambazo tayari zipo katika soko.
Kampuni ambayo imetengeneza simu hii sio mpya na inakwenda kwa jina la Nubia. Kampuni hii inatengeneza simu za muendelezo wa RedMagic mahususi kabisa kwa ajili ya magemu.
Simu hii inakuja na prosesa ya Snapdragon 8 Gen 2 ambayo inafanya kazi zaidi ya kampuni ilivyotegemea, inakuja na feni ya kupoozea joto na betri kubwa (lenye uwezo mkubwa).
Kampuni pia ina toleo la RedMagic 8S Pro Plus ambalo lina 24GB RAM na ujazo uhifadhi wa ndani ukiwa unafika 1TB.
Pengine kwa sasa hii ndio itakua simu yenye uwezo zaidi maana haina mpinzani katika vipengele tajwa ingawa kuna simu ambazo zina uwezo mkubwa na pia ni mahususi kwa ajili ya magemu.
Betri yake ni yenye uwezo wa 6,000mAh na inatumia 80W katika chaja yenye uwezo wa kuchaji kwa haraka (fast charge).
Kwa uwezo huo tuu ni kwamba hapa utafurahia magemu mbalimbali bila ya kutokea kasoro yoyote ya kukutoa katika mchezo kama vile kuganda ganda.
Kifaa hiki pia kinakuja na kamera tatu huku mpaka sasa kampuni imeweka wazi uwezo wa kamera moja tuu ambayo ni kuu na ina 50MP.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, je unadhani ni sawa kwa sasa kwa simu kuja na uwezo wa RAM 24GB au wamewahi sana?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.