Kuna matoleo kadhaa ya toleo la simu janja ndogo kutoka Samsung ifahamikayo kama Samsung Galaxy Star Pro. Leo tutazama toleo la GT S7262 ambalo ndio hasa linapatikana katika nchi zinazoendelea, pamoja na Tanzania.
Kwanza kabisa fahamu ya kwamba simu hii ni ya bei nafuu sana na inalenga kwa watu wenye bajeti ndogo sana ya simu ila wanataka simu inayotumia Android.
Ni simu yenye ukubwa wa inchi 4 (display) na inakuja na uwezo wa laini mbili za simu.
Sifa zingine ni pamoja na prosesa ya GHz 1, RAM ya MB 512 pamoja na diski uhifadhi (storage) wa GB 4 tuu. Ingawa GB 4 ni ndogo kuna uwezo wa kutumia memori kadi ya hadi GB 32.
Samsung Galaxy Star Pro inakuja na Android 4.1 pamoja na betri la mAh 1500…kwa udogo wake kiwango hiki cha chaji kinategemewa kudumu muda mrefu tuu.
Sifa kwa ujumla
- Display – inchi 4.00
- Prosesa – GHz 1
- Kamera ya selfi – Hakuna
- Kamera kuu – Megapixel 2
- Resolution 480×800 pixels
- RAM – MB 512
- OS – Android 4.1
- Diski Uhifadhi – 4GB
- Betri – mAh 1500
Bei? Simu ya Samsung Galaxy Star Pro inapatikana kwenye kati ya Tsh 75,000/= hadi 95,000/= hivi.