Je, katika simu za 2019 ulizozipenda kuna ambazo zinaweza zikawa kwenye orodha ya simu 10 zilizouzika zaidi kwa mwaka huo?
Hii ni orodha ya simu zilizofanya vizuri zaidi sokoni kwa mwaka 2019. Data hizi ni kulingana mauzo ya simu, na ni data zilizothibitisha na vyanzo mbalimbali. Kikubwa katika orodha hii ni kwamba Samsung na Apple wameingiza simu tisa kati ya kumi zilizo kwenye orodha hii. Ukiangalia utagundua pia kuna simu zilizotoka miaka ya nyuma ya 2019 lakini bado ziliuzika sana mwaka huo, mfano iPhone 8 ilitoka 2017
Namba moja: iPhone XR

Simu ya iPhone XR ndiyo simu iliyoshika namba moja katika orodha hiyo. Na imepita simu iliyoshika namba mbili, iPhone 11 kwa takribani asilimia 1 tuu.
Orodha nzima na simu zingine zilizoingia kwenye orodha ya simu 10 zilizouzika zaidi na kiasi zilivyoshika soko kimauzo kwa mwaka huo – kiasilimia.
Namba moja – Apple iPhone XR
Idadi ya iPhone XR zilizouzika ni asilimia 3 ya mauzo yote ya simu janja mwaka 2019.
—
Namba 2 – Apple iPhone 11
Asilimia 2.1
—
Namba 3 – Samsung Galaxy A50
Asilimia 1.8
—
Namba 4 – Samsung Galaxy A10
Asilimia 1.7
—
Namba 5 – OPPO A5 (2019)
Asilimia 1.3
—
Namba 6 – Apple iPhone 8
Asilimia 1.2
—
Namba 7 – Samsung Galaxy A20
Asilimia 1.1
—
Namba 8 – Apple iPhone 11 Pro Max
Asilimia 1.1
—
Namba 9 – Apple iPhone 7
Asilimia 1.1
—
Namba 10 – Apple iPhone XS Max
Asilimia 1.0
Kama unavyoona nafasi 6 zimechukuliwa na Apple wakati Samsung wamechukua nafasi 3. Simu za hadhi ya kati kama vile Samsung Galaxy A20 na A50 zinaonekana kufanya vizuri zaidi kimauzo kwa Samsung kuliko h0ata simu zao za hadhi ya juu zinazoshindana moja kwa moja na simu za iPhone.

Data zinaonesha pia kwa barani Africa na Mashariki ya Kati Samsung ndiye aliyechukua nafasi tano za juu za mauzo ya simu ambapo simu za Samsung Galaxy A10, A2 Core, A50, A20 na A10s ndizo zilizouzika zaidi.
Kwa Marekani nafasi zote tano za juu zilichukuliwa na Apple kupitia iPhone XR, 11, 8, 11 Pro Max na XS Max. Kwa Ulaya Samsung ndio iliongeza, nafasi ya kwanza ilichukuliwa na Samsung Galaxy A50, nafasi ya pili na tatu zilienda kwa Apple kupitia iPhone XR na 11 wakati nafasi ya nne na tano zilirudi kwa Samsung kupitia Galaxy A10 na A40.
Data hizi zinaonesha bado Apple amelishikilia vizuri soko la simu za hadhi ya juu – hasa Marekani (moja ya soko kubwa la simu janja), ila pia inaweza ikaonekana suala hili linasababishwa na Samsung kuwa na simu nyingi sana ata kwa zile zenye uwezo wa juu wa kushindana na za Apple.