Simu nyingi za Huawei ambazo zipo tayari sokoni zinazotumia Kirin (kipuri mama) ni chache ukilinganisha na zile ambazo zinatumia aina nyingine ya vipuri lakini hilo linatazamiwa kubadilika katika nusu ya pili kwa mwaka 2019.
Huawei wamekuwa wakinunua vipuri mama kutoka kwa makampuni mbalimbali na kutumia kwenye simu janja wanazotoa kulinganisha na zile ambazo zimewekwa Kirin ikiwa kama ndio “Ubongo” wa simu husika. Mambo yanatarajiwa kuwa tofauti kidogo hasa kwa simu janja ambazo zitatoka kwenye robo ya pili mwaka huu; kwa lugha rahisi zitatumia Kirin zaidi badala ya Qualcomm.
Takwimu zinaonesha kuwa nusu ya pili mwaka 2018 Huawei walitumia pungufu ya 40% kwa vipuri vya Kirin SoCs wanavyotengeneza wao wenyewe huku nusu ya kwanza mwaka 2019 walitumia kipuri cha Kirin kwa 45%. Sasa kwa robo ya pili zaidi ya milioni 150 za simu za Huawei zitatumia kipuri cha Kirin huku ikiwa na mpango wa kuuza maeneo mbalimbali simu janja 270 milioni mwaka huu ambapo hiyo yote ni sawa na 60%.
Huawei wameamua kuweka nguvu kubwa zaidi kwenye kipuri wanachotengeneza weyewe kwa sababu ya kutaka kupunguza utegemezi kutoka kwa makampuni mengine mathalani wanaotengeneza MediaTek na Qualcomm.
Ndio hivyo Huawei wameamua kutumia vya kwao zaidi na hivi karibuni wametoa Kirin 810 sasa basi tutegemee kuona simu janja nyingi zikitumia vipuli vya kwao zaidi.
Vyanzo: GSMArena, Tech Lapse