Kampuni ya Kifaransa ya mawasiliano ya Orange ambayo inafanya kazi katika nchi 21 za Afrika ikiwemo Kenya inategemea kuleta simu-janja za bei nafuu zaidi kwa mamilioni ya waafrika ambao kwa sasa wanatumia na wanaweza kununua simu za mkononi za msingi. Simu hii inaitwa OrangeĀ Klif.
Klif, illitangazwa kwa mara ya kwanza mjini Barcelona kwenye Maonesho ya Mawasiliano ya Mkononi (Mobile World Congress show) na imetengenezwa kwa ushirikiano wa asasi ya Mozilla na kampuni ya Alcatel OneTouch.
Klif inaendeshwa na mfumo-endeshaji wa Firefox OS, ambao umetengenezwa juu ya mfumo wa kivinjari cha Firefox kwa kutumia mfumo wa Linux ambao ulitumika kuanzisha Androidi.
Mozilla wanalenga biashara ambayo bado haijafikiwa na mifumo mingine, kwani Androidi, windows na wengine hawajajizatiti vya kutosha kuhudumia watu ambao hawapo tayari kutumia kiasi kingi cha fedha kuungwa na intaneti. Kwa hiyo, katika kufanya hili Firefox na Alcatel wanajivunia kupanua wigo wa intaneti.
Ingawa inaonekana kwamba watu wengi wana simu-janja siku hizi ila bado chini ya 10% ya watu chini ya jangwa la Sahara wanatumia simu hizi na kuna uwezekano simu kama za Firefox OS zinaweza kuongeza idadi ya watu.
Intaneti inatajwa na wanataaluma na watu mashuhuri duniani kama nyenzo muhimu ya kujikwamua kimaisha kwa kuondoa ujinga na kuwezesha watu.
Orange wanatoa MB 500 kila mwezi kwa miezi sita na pia dakika za maongezi pamoja na simu za Klif. Orange wanatazamia kwamba jambo hili litawavutia wateja kujipatia simu za Klif na kusambaza mfumo-endeshaji wa Firefox OS.
Sifa za Simu ya Kliff
- Klif inatumia laini mbili.
- Kioo cha inchi 3.5 (HVGA)
- Intaneti ya 3G
- Kamera ya MP 2
- Uhifadhi wa MB 512
- Kumbukumbu (RAM) ya MB 256
- Betri ya mAh 1300
- Prosesa ya MediaTek ya GHz 1
Simu hizi zinatazamiwa kuendana na soko la Afrika kwani hazina masharti ya kusajili kwa barua-pepe ili kupata huduma za ziada na inaweza kutumika bila kuhitaji ujunzi mkubwa wa teknolojia. Bei yake itaanzia kwa Dola za Kimarekani 40 (Elfu 75 za Kitanzania). Pia, uwezo wa kutumia laini mbili unandana sana na soko. Firefox OS imefanikiwa sana katika nchi za Amerika ya Kusini na baadhi ya nchi za bara la Asia na sasa simu zake zinanukia Afrika na Mashariki ya Kati.
Je, unadhani juhudi za Mozilla kuwawezesha Waafrika kwa simu za FirefoxOS za bei nafuu zaidi na uwezo wa msingi kwa ajili ya intaneti zitafanikiwa?
Picha Na:
No Comment! Be the first one.