WhatsApp mara kwa mara imekua ikitoa vipengele kadha wa kadha katika kuhakikisha kuwa huduma yake inaimarika Zaidi.
Licha ya WhatsApp kuwa na vipengele vingi, bado huduma yake inakua ni moja kati ya huduma muhimu na zenye watumiaji wengi.
Kampuni inaonyesha dhahiri kwamba inawkeza nguvu nyingi katika kuhakikisha watumiaji wake wanapata kile kilicho bora na wanafanya hivyo kwa kuongeza vipengele vizuri.
Kwa watumiaji wa Android kwa sasa wanaweza furahia kipengele hiki kipya ambacho kitawawezesha watumiaji hao kuweza kupiga simu kwenye kundi huku washiriki wakifikia mpaka 31.
Kuna muda katika makundi hayo waliweza shiriki watu 15 katika simu hiyo lakini kwa sasa hilo limebadilika na sasa ni namba kubwa Zaidi.
Kipengele hiki kwa sasa kinapatikana kwa watu kadhaa tuu ambao wamechaguliwa kuganyia kipengele hicho majaribio.
Kwa kuanzia wameanza na watumiaji wa Android lakini inaonekana dhahiri kwamba kipengele hicho kitamfikia hata mtumiaji wa iPhone huko mbeleni.
Kingine ni kwamba WhatsApp pia imeboresha swala zima la ulinzi na usalama na hii ni katika kuhakikisha tuu kwamba watu wanakua na uhakika wa usalama wa mazungumzo yao.
Ni wazi kabisa moja kati ya sifa kubwa ya WhatsApp ni kuweka kipaumbele katika swala zima la ulinzi na usalama wa mazungumzo baina na mtu na mtu.
Nianfikie hapo chini katika eneo la comment, je unadhani ni sawa kwa WhatsApp kuendelea kuongeza namba hiyo ya washiriki katika simu hizo za makundi?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.