Hapo zamani simu za mikononi zilikua zikishutumia kuwa ni moja kati ya visababishaji vikuu vya kansa na sio tiba ya ugonjwa huo. Mida imebadilika na mambo pia yamebadilika Taasisi ya Marekani The Nation Cancer Institute imetoa uoga huo kuhusianana matumizi ya simu kwa watu. Na sasa simu-janja (smartphone) zetu zinaweza kutusaidia kugundua Saratani na kujua njia mbalimbali za kujikinga nayo.
Mwezi Oktoba ni Mwezi wa ufahamu wa saratani ya Matiti duniani. Katika akili yangu nafikiri mwezi huu ni mwezi wa akina mama wote kujitolea kupima kwa wingi. Pia ni mwezi wa wale wenye uwezo kuchangia taasisi, hospitali na vyombo mbalimbali vinavyopingnana na ugonjwa huu, Ndio! Misaada pia inasaidia. Jamii ya watu wa teknolojia na watafiti wamekutani ili kwenda mbele zaidi ya awali kwa kutafuta tiba ya Saratani kwenye simu-janja yako!
Siku Ya Apple
Kwa mwezi Oktoba Kampuni Ya Elektroniki (Apple Inc) imeanzisha mfuko ambao watumiaji wa vifaa vyake kama simu, kompyuta na tableti wataweza changia ili kudhibiti ugonjjwa wa Saratani. Michango hiyo itaenda yote (100%) kwenye Kampuni nguli duniani ya utafiti wa Saratani City Of Hope kupitia iTunes. Wewe ndio unachagua kiasi cha kutuma _ dola 5, dola 10, dola 15, dola 25, dola 100, dola 200_ hiyo itatoka kwenye akaunti yako ya iTunes. Apple Hawatachukua hata thumni ya mchango huu. Hii ni njia rahisi sana ya kuchangia ili kutafuta tiba ya Saratani pia ni dili kubwa sana kwa kampuni ya Apple. Mwezi wa Oktoba pia unaashira kumbukumbu ya kifo cha mwanzilishi wa kampuni ya Apple Steve Jobs maana alifariki dunia Mwezi Oktoba mwaka 2011 sababu ya Saratani.

Gemu La Genes In Space
Ukiongelea vya kusangaza, Shangaa na hii. Wanasayansi wamejitolea maisha yao na kuweka juhudi katika kutafuta tiba ya Saratani. Pia wana data kibao kwenye vichwa vyao zisizoaminika kwa watu wa kawaida na ni binadamu wachache sana wanaweza kuzisoma data hizo. Hapo ndio wewe na simu yako mnapoingia.
App ya Genes In Space inakuwezesha wewe kutafuta tiba ya kansa katika mfumu wa gemu la simu. Gemu hilo halina tofauti sana na magemu mengine ya angani. Pale unavyokwepa vimondo na mambo mengine hatarishi, bila kujijua unasaidia kutafuta njia zingine za kusaidia na kutafuta tiba ya Saratani. Gemu hili lilikua ni ndoto ya Cancer Research ya marekani pia ni ya 100% bure katika iOs na Android

Sasa Linasaidia vipi kutibu Saratani? Jibu ni rahisi sana kuliko unavyofikiria: Gemu imetafsiri data za utafiti wa Saratani na kuwa vitu vinavyopaa kuelekea kwenye ndege yako. Vile inavyokusanya Vitu vinavyohitajika ili kupata pointi ili ushinde Gemu hilo unasaidia wanasanyansi kujua data ambazo wanaweza tumia ili kutibu Saratani katika hali ya Ukweli na ya kawaida.
B4BC
B4BC inasimama badala ya ‘Boarding For Breast Cancer’. Hii ni taasisi isiyo ya kujipatia faida kwa kazi na huduma wanazotoa kwa jamii. Taasisi hii inasaidia wanawake wote na jamii kwa ujumla kwa kutoa mafunzo na ujuzi kuhusi Saratani ya Matiti. Pia imetokea taasisi hii kuwa na App katika store za iOs na Android pia imetengenezwa spesho kwa wanawake walio bize katika maisha yao.

Jifunze jinsi ya kujifanyia mitihani kuhusu saratani mwenyewe bila kuwa na dokta, kuangalia mbinu za kila siku za kukuwezesha kubaki na afya nzuri, hata kuweka alamu ya mwezi ili kukukumbusha kujifanyia ‘check up’ mmwenyewe ili isije ikaingiliana na ratiba zingine za kila siku.
App Ya DermoScreen
Sio kila siku watu kama wewe au mimi wanaweza kutumia Aplikesheni za simu janja kutibu na kuzuia saratani, Daktari anaweza ingia kwenye zoezi hili pia. App ya DermoScreen inafanya kazi na kifaa kingine ambacho ni kamera ambayo iko spesho kupima Saratani ya ngozi

Profesa wa chuo cha Huston, Texas ametengeneza hii App kwa lengo la kusaidia madokta kuona uwezekano wa kuwa na saratani ya ngozi kwa wagonjwa. Unaweza ukawa unajiuliza ni kiasi gani iko sahihi? Jibu ni kwamba, kwa kiasi kikubwa. Kwa kutumia simu janja (simu hiyo hiyo unayotumia kupiga na kutuma meseji), vipimo mara ya kwanza vilionyesha kuwa App iligundua 80% ya usahihi wa Saratani ya Ngozi kwa mda huo.
Wakati dunia ikibalika hatuna budi kubadilika nayo, tukifuatilia hayo hapo juu itatuwezesha kushinda Saratani au unaonaje? Ningependa kusikia kutoka kwako! . Comment kwenye kiboksi hapo chini.
No Comment! Be the first one.