Ubunifu wa siti za ndege za ghorofa uliooneshwa kwenye maonesho ya sekta ya ndege yanayokwenda kwa jina la Aircraft Interior Expo yalifanyika mwezi Juni mwaka huu, uliwavutia wengi huku ukileta maswali kwa wengine.
Kwa miaka mingi teknolojia ya ndege imebadilika kwa kiasi kikubwa ila sehemu moja ambayo bado wasafiri wanalalamika haijawa nzuri kwao ni kwenye siti na ukaaji wake – viti vimebanwa karibu karibu na hivyo kuzuia uwezo wa kuvilaza nk, na hivyo kufanya hali ya usafiri wa raha kubakia kwa wale wanaotumia ndege kubwa, na tena wanaokata siti za daraja la juu zaidi (gharama).
Kupitia ubunifu huu kampuni inayotokea katika jiji la Madrid linaenda kwa jina la Chaise Longue linalenga kuraisisha uwezo wa kutopunguza idadi ya abiria kwenye ndege, bali kuongeza uwezo wa abiria kufurahia zaidi safari yao kwa uwezo wa kujinyoosha vizuri kwenye siti zao ukilinganisha na hali ilivyo sasa.
Ubunifu wa upangaji wa siti huu unahisha kuongeza nafasi zaidi kwa watu kuweza kukaa kwa kutumia nafasi ya chini na juu katika upangaji wa viti.
Faida zake:
Siti ni nyepesi zaidi kuliko zinazotumika kwa sasa, na hivyo kuleta faida kwa waendeshaji ndege kwani kwa kila kilo zinazopungua kwenye uzito ndege ndivyo pia ulaji mafuta unavyopungua.
Siti za chini zinafikika kwa urahisi zaidi, na kuwapa wapitaji nafasi zaidi ata ya kuweka vitu. Nafasi ya kunyoosha miguu hasa kwa wanaokaa viti vya chini ni kubwa ukilinganisha za kwa sasa.
Changamoto:
Usambaaji wa hewa.
Kwanza: Kama ikitokea abiria aliyekaa eneo la chini akiachia gesi chafu (kijamb*), italeta usumbufu sana kwa watu waliokaa eneo la juu kwani hewa ya joto itawahi kupanda juu kwa haraka zaidi.
Pili: Mfumo wa sasa wa usambazaji hewa ndani ya ndege umebuniwa kwa kutegemea ubunifu wa sasa wa siti za ndege – kumaanisha zimeacha nafasi kubwa eneo la juu ya siti. Ili siti hizi zipate ruhusa ya kutumika itabidi utafiti zaidi katika suala la usambazaji hewa, na utoaji wa mifumo ya kuvutia hewa ya dharula kufanyika.
Maeneo ya mizigo
Ubunifu huu unaondoa sehemu za kuwekea mizigo zilizoeleka eneo la juu, pembeni, katika pande zote mbili za ndege. Wateja itabidi wabaki na eneo la chini ya siti tuu kwa ajili ya uwekaji wa mizigo midogo wanayoingia nayo kwenye ndege.
Tayari kampuni hiyo inashirikiana na vyombo vinavyohusisha upitiaji na utoaji wa vibali vya teknolojia kama hii kutumika.
Kwa mtazamo wako unauonaje ubunifu huu? Tuambie kwenye comments, usisahau kushare.
Teknokona / Habari za sekta ya ndege na anga
Chanzo: offthebeatenpoints.com na vyanzo vingine mbalimbali
No Comment! Be the first one.