Kupitia toleo la Starship la SN10 kwa mara ya kwanza kampuni ya SpaceX imefanikiwa kurusha juu na kuitua tena roketi ndege yao kwa mafanikio makubwa.
SpaceX ni kampuni iliyojikita katika kufanikisha safari za anga kwa gharama nafuu, na ili kuwezesha kufanikiwa wanawekeza katika kuja na roketi ndege itakayokuwa kuwa na uwezo wa kufanya safari za anga – hapa duniani, safari za duniani kwenda mwezini na za hadi safari ya Mars. Ili kufanikisha ili sifa kubwa ya roketi ndege hii ya familia ya Starship ni kuwa na uwezo wa kutumika mara kwa mara bila uhitaji wa matengenezo makubwa.
Kwa kipindi kirefu vifaa vya safari ya anga vilikuwa vinavyotumika mara moja tuu, na hivyo kufanya gharama za safari hizo kuwa juu sana. Fikiria mfano kama ndege mpya ingekuwa inaweza kutumika mara moja tuu kwa safari moja, kutokana na gharama kubwa ya utengenezaji jambo hili lingefanya tiketi zake kuwa za bei ghari sana. SpaceX wanataka kufanya pia vyombo vya usafiri wa anga za juu kuwa vinavyoweza kutumika mara nyingi zaidi, na hili litasaidia kushusha gharama zake.
Katika jaribio la tatu roketi hiyo iliweza kufanikiwa kutua kwa usalama, zingine zote mbili za kabla ya jaribio hili zililipuko katika hatua ya utuaji. Ila baada ya kutua ilionekana kulikuwa na moto unaendelea kuwepo eneo la moja ya miguu yake, na hivyo dakika kama 4-8 baada ya utuaji salama roketi ndege hiyo ililipuka. Kwa sababu za kitafiti bado lengo kuu lilikuwa kuwezo kuonesha uwezo wa kuitua roketi hii na hivyo limefanikiwa, tayari SpaceX wanaroketi nyingine ya SN11 ipo tayari kwa majaribio zaidi.
Tutegemee SpaceX kuchukua data za majaribio haya katika kuboresha toleo la SN11. Kwa muda mrefu hicho ndio kinachosukuma tafiti na utengenezaji wao wa roketi, hawaogopi matatizo/kukosea, wanayachukulia kama sehemu ya kujifunza zaidi na kuboresha zaidi.
Soma zaidi kuhusu;
- SpaceX – Teknokona/SpaceX
- Masuala ya Anga – Teknokona/Anga
No Comment! Be the first one.