Mtandao wa Snapchat licha ya ukubwa wake wote, mtandao huu wa kijamii ulikua haupatikani katika katika soko la App la Microsoft Store.
Ukiachana na App katika vifaa kama simu na tabiti bado Snapchat ilifanya maboresho katika Snapchat ya mtandao ili angalau iendane na App ya kwenye simu lakini bado kuna baadhi ya vitu havikuendana.
Kwa sasa App inapatikana katika kompyuta ambazo zinatumia programu endeshaji ya Windows na soko ambalo linatumika ni Microsoft Store.
Hii linatokea ikiwa imepishana kidogo sana na App ya WhatsApp ambayo nayo imeanza kupatikana ndani ya miezi michache katika soko hilo la Apps.
Ni wazi kwamba kuna App nyingi ambazo bado hazijaanza kupatikana katika soko la Microsoft Store na nyingi zinafanya mpango ili kuanza kupatikana katika soko hilo.
#Snapchat, which avoided the #Windows platform with no official apps or support, has finally arrived on the Microsoft Store as a Progressive Web App.
According to Windows Central, Snapchat's Progressive Web App (PWA) will run through Microsoft Edge on Windows 10 and 11 PCs. pic.twitter.com/sfMJHi024C
— IANS (@ians_india) November 27, 2022
Ni wazi kwamba mtandao huu ulikua unasubiriwa kwa hamu sana kwa miaka na miaka katika soko hili na sasa imekuja huku App yenyewe ikiwa na ukubwa wa 1.4MB.
Kwa kupitia Snapchat ya jukwaa hili basi utakua na uwezo wa ku’chat, kuangalia ‘stories’ na hata uweza wa kupigia simu ndugu, jamaa na marafiki.
Kingine ni kwamba App hii iko katika mfumo wa PWA (progressive web application) na kama inavyojulikana ni kwamba mfumo huu wa App unamaanisha kuwa …
….App zinakua ni za mtandao lakini zinakua na sifa zote sawa na App ambazo zinapatikana katika simu janja.
Ningependa kusikia kutoka kwako,je unaweza kutumia mtandao wa Snapchat katika kompyuta yako? Au ndio umeshazoea mtandao huo katika simu jnaja tuu?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.