Mtandao wa Snapchat ambao ni gumzo hapa mjini umeingia katika vichwa vya habari vya teknolojia baada ya taarifa kwamba upo katika mpango wa kuinunua kampuni iliyotengeneza Bitmoji kuvuja.
Bitstrips ni kampuni ya kutoka Toronto iliyotengeneza bitmoji mwaka 2012, Bitmoji ilikuwa maarufu kwa haraka katika Facebook kwa kuwaruhusu watumiaji wake kutbadili picha zao kuwa emoji.
Snapchat wenyewe walipoulizwa juu ya dili la kuinunua Bitstrip walikataa kusema chochote juu ya hilo na hii inanipa imani kwamba hili dili ni kweli lipo. Tetesi ni kwamba Snapchat watainunua kampuni hii kwa kiasi cha dola za kimarekani milioni mia moja.
Hii ni habari nzuri kwa watumiaji wa Snapchat ambao wamekuwa wakifurahia utimiaji wa emoji maana tunategemea siku zijazo tutaanza kuona mbwembwe za Bitmoji katika Snapchat na hivyo tutakuwa na sababu nyingine ya kusnapchat.
Kwa Snapchat hii ni nafasi nyingine ya kuwavutia watumiaji wapya kitu ambacho ni muhimu saana kwa mtandao wa kijami, pia hii ni nafasi ya Snapchat kuhakikisha kwamba watumiaji wake wa zamani hawawi bored.
Kwa Bitstrip hii ni nafasi yao kutoa huduma kwa watumiji wengi zaidi ambao pengine ingechukua muda mrefu saana kuwafikia ama kuwapata, pia dola milioni mia moja zinaweza kufanya mambo mengi kwa wamiliki wa kampuni hii.
Sekta ya teknolojia ya Tanzania inayomengi ya kujifunza kutoka katika ma dili kama haya, makampuni makubwa yasiogope kuyanunua makampuni madogo ya teknolojia na vivo hivo makampuni madogo ama start-ups zisiogope kununuliwa ila tu yahakikishe kwamba yananufaika na dili husika.
Endelea kuwa nasi kwa taarifa zote ta teknolojia katika lugha ya Kiswahili.
One Comment
Comments are closed.