Snapchat ambayo inapendwa na wengi ulimwenguni kutokana na mtandao huo ulioanzishwa mwaka 2012; thamani ya mtandao huo imezidi kupanda.
Kwa zaidi ya miaka minne ya kujiendesha kama kampuni bila kutegemea pesa yoyote ile kutoka kwa watu wengi kama vile wanahisa hivi karibuni Snapchat iliamua kujiunga na soko la hisa la jijini New York.
Hisa za Snapchat ziliuzwa kwa matajiri kutoka New York kwa kiasi cha dola bilioni 24. Snapchat ni kampuni ya pili kujiunga katika soko la hisa la ‘Wall Street’ ambalo ni kubwa; mtangulizi wake akiwa Facebook.

Snap Inc kampuni mama inayomiliki programu tumishi ya Snapchat ilianza biashara kwa kuanzisha app ambayo meseji zilikuwa zikitokea baada ya kuwa zimeshakwishasomwa. Snap Inc ilifanikiwa kuuza hisa zake zote jumla ya 200 milioni kwa dola 17 kila moja.
Snapchat ambao waonekana wakijisogeza karibu zaidi na wateja wake wakionekana kutengeneza miwani janja yemye kamera iliyo ndani kwa ndani; miwani hiyo inaitwa Spectacles. Awali Snap Inc ililenga kupata kati ya $19.5 bilioni na $23 bilioni.
Kwa sasa wananchi na wawekezaji mbalimbali wanaweza kuwa moja ya wamiliki kampuni hiyo kupitia soko hilo la hisa, changamoto kubwa kwa Snapchat ni kuonesha hali ya kuleta faida.
Hadi sasa app hiyo haijatengeneza faida yeyote ila tayari inaingiza mapato yanayoonesha yanakua kwa kiasi flani na wengi wanaamini bado app hiyo inaweza kuongeza idadi ya watumiaji na kutengeneza pesa nyingi kupitia matangazo.