Solar Impulse 2 ndege ambayo inatumia umeme jua kwa asilimia 100 imefaikiwa kutua nchini Uhispania kukamilisha safari ya kihistoria ya kukatisha bahari ya Atlantiki, safari ambayo ilichukua takribani masaa 70 katika kukamilisha misheni yake ya kuzunguka ulimwengu.
video ya solar impulse 2 ikiruka huko Dubai mwakajana kuanza safari
Awali ndege hii ilikuwa itue Ufaransa ili kumuenzi Charles Lindbergh ambaye akiwa na ndege yake aliweza kufanya safari ya kwanza ya ndege kuvuka bahari ya Atlanitiki lakini kutokana na hali ya hewa mpango huu wa Solar Impulse 2 uliingea dosari na ikabidi kwenda kutua jijini Sevila nchini Hispania ambako hali ya hewa ilikuwa salama kutua.
Kwa mujibu wa FOX news ndege hii ina mabawa ambayo ni mapana kushinda aina ya ndege tulizozizoea na ina ingini mbili katika kila bawa ambazo zinaendeshwa na nguvu ya umeme jua unaokusanywa katika mabawa yake.
Solar impulse 2 inaupana wa mita 72 huku ikiwa na uzito wa tani mbili nukta tatu na inakwenda kwa mwendokasi wa kilomita 70 kwa saa.

Safari hii ambayo ni ya umbali wa karibu kilomita 6765Km ilichukua karibu siku tatu yaani masaa 71 na dakika nane, ingawa siyo lengo la Solar Impulse kuleta ndege ambazo zitakuwa zinatumia umeme jua lakini ni wazi kwamba mafanikio ya safari hii yatakuwa chachu kwa watengenezaji wa vyombo vya usafiri wa anga kuangalia uwezekano wa kubadili namna ambayo injini za ndege zimekuwa zikiendeshwa.
Kwasasa ndege zinaendeshwa na nishati ya mafuta ambayo ni nishati ainayoweza kuisha na pia sio rafiki kwa mazingira, kwa upande wa jua hiki ni chanzo rafiki kwa mazingira na pia ni chanzo mbadala cha nishati.
Ndege hii inaupana wa mita 72 huku ikiwa na uzito wa tani mbili nukta tatu na inakwenda kwa mwendokasi wa kilomita 70 kwa saa.