Hakuna mwanga wa jua? Ondoa shaka, sasa kuna uwezekano wa Solar Panel zinazokuja kuweza kufua umeme si kwa kutegemea mwanga wa jua pekee bali hadi matone ya mvua.
Kwa miaka mingi teknolojia ya Solar panel imekuwa ikitegemea miale ya jua katika ufuati wa umeme, lakini kupitia watafiti wanasayansi wa nchini Uchina teknolojia hiyo inaweza pata maboresho makubwa.
Kwa sasa solar panels zinafua umeme vizuri zaidi muda wa asubuhi hadi jioni anga ikiwa nyeupe bila mawingu mazito. Pale panapokuwa na mawingu basi umeme huwa unafuliwa kwa kiwango kidogo zaidi kwa kadi ya asilimia 10 – 25 ukilinganisha na pale anga inapokuwa nyeupe ikiruhusu mwanga wa jua zaidi.
Kupitia watafiti wa nchini Uchina, sasa umeme utaweza kufuliwa kwa kiwango kikubwa ata katika kipindi cha mvua kali.
Inafanyaje fanyaje kazi?
Wanasema katika solar panels hizi kuna ngozi imewekwa juu yake iliyotengenezwa kwa kutumia ‘electron-enriched graphene’ ambayo hufua umeme pale inapokutana na ‘ions’ zilizokwenye matone ya mvua.
Ubunifu huu umefanyika katika Chuo kikuu cha Ocean, chini ya uongozi wa Profesa Qunwei Tang
Bado haijajulikana itachukua muda gani kwa teknolojia hiyo kuingia madukani ila inaonekana bado itaitaji maboresho kadhaa kabla ya kuanza kutumika maviwandani katika kutengeneza solar panels.
Una maoni gani?
Vyanzo: Telegraph na vyanzo mbalimbali
One Comment
Comments are closed.