Teknolojia ya umeme wa sola inazidi kukua kwa kiasi kikubwa sana siku hizi. kuna kampeni zinazoongozwa na kampuni ya Kickstarter, kampuni hiyo kupita kampuni inayoitwa Yolk imesubutu na kuleta teknolojia ya chaja ya simu inayotumia sola. Chaja hii inaitwa ‘Solar Paper’, pia inasemekana ndio chaji ya sola yenye umbo dogo kuliko zote.
Chaja hizo (Solar Paper) zipo za matoleo manne na zinatofautiana kwa baadhi ya vitu na hata kiasi cha umeme (watt). Watengenezaji wa chaja hizo wanasema ikiwa juani chaja hiyo inaweza kuchaji iPhone 6 kwa masaa mawili na nusu na ukifikiria hiyo ni sawa na chaja ya ukutani tuu.

Chaja ya Solar paper ni ndogo sana kiumbo lakini hiyo sio sababu tuu ya uuzaji wake. Solar paper itaacha kuchaji simu yako pale itakapokosa jua na itaendelea kuchaji pindi itakapopata la kutosha.
Chaja (Solar Paper) zinapatikana katika makundi manne tofauti ambayo yanahusisha tofauti kati ya namba za ‘panel’. Kila panel inawakilisha 2.5W. Hii inamaanisha ile ya kundi la 5W ni panel mbili tuu, ya kundi la 7.5W ni panel 3 na hata ile ya kundi la 10W ni panel nne.
Solar Paper Ile ya 2.5W kama ilivyooelezwa kuwa haifanyi/haitaweza kuchaji simu janja bali itakuwa na uwezo wa kuchaji betri la ziada tuu. Ile ya 7.5W ndio sahihi kwa kuchaji simu janja kwa kuwa inaweza hata kuchaji iPhone 6 kwa masaa mawili na nusu tuu. Na ile ya 10W inasjhauriwa kuchaji kwa vitu kama vile iPad na tabiti zingine.

No Comment! Be the first one.