Sony ni moja kati ya chapa kubwa sana katika ulimwengu wa teknolojia, chapa hii ina bidhaa nyingi halikadhalika na bidhaa ya simu.
Kwa haraka haraka ni kwamba kwa upande wa simu kampuni ya Sony haifanyi vizuri sana kama zamani lakini hiyo haimaanishi kwamba kampuni halina wateja katika soko.
Ni makampuni mengi sana yalikua yanafanya vizuri katika soko la simu janja lakini mwishoni hali ilibadilika na kuachana kabisa na biashara hiyo.
Sony wao bado hawajafikia huko, na kwa taarifa ambazo zipo ni kwamba kampuni imejitoa kutengeneza simu zingine kadhaa kwa miaka ijayo.
Hii inamaanisha kwamba bado kampuni itabaki katika soko na itaendelea kupiga kelele na kuwa mshindani mkubwa tuu katika Nyanja hiyo.
Kwa mujibu wa Qualcomm ni kwamba makampuni hayo mawili yameingia katika makubaliano ambapo Sony atatengenezewa chip (chipsets) nyingi (za simu tofauti tofauti) huko mbeleni.
Japokua hawajaweka wazi kila kitu kama vile miaka n.k lakini ni kwamba simu hizo ni zile za hadhi ya juu kabisa na zile za hadhi ya kati.
Chip hizo zitakua zile zinazojuliakana kama Snapdragon chipsets. Hii inaonyesha wazi kwamba Sony bado inaikubali kampuni ya Qualcomm ndio maana wako radhi kuendelea nao kwa miaka kadhaa.
Kumbuka Xperia 1 V ilikuja na chip ya Snapdragon 8 Gen 2 na ilikua ni simu shindani kabisa katika soko licha ya kufanya vibaya maana haikufikia kwenye umaarufu huo.
Pengine labda kampuni ya Sony imejiwekea miaka kadhaa pengine inaweza ikaanza kushindana jino kwa jino na makampuni kama vile Apple na Samsung.
Wengi bidhaa ya simu kwa Sony hawaioni ikiendelea, lakini Sony wao wanayo ya kwao kichwani na kwa sasa inaonekana kwamba wanakomaa nayo mpaka mwisho.
Ningependa kusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini katika upande wa comment, je unalichukulia kampuni la Sony katika biashara ya simu janja? Je itawashinda?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.