Sony na Honda kupitia katika ushirika wao wa toka mwaka 2022 kwa sasa wako katika mchakato wa kuja na gari ambalo linatumia nishati ya umeme, Gari hilo linakwenda kwa jina la Afeela.
Kwa mara ya kwanza kabisa mfano wa gari hii (Afeela) umeonyeshwa au kuzinduliwa rasmi katika mkutano wa maonyesho yaa CES 2023 (consumer electronics show 2023) ambao umefanyika januari hii.
Kwa haraka haraka inasemekana kwamba gari hii ya umeme itakua na sensa za kutosha ambazo kwa namna moja au nyingine zitasaidia katika uendeshwaji wa gari hilo.
Kumbuka kampuni ya Honda imejikita zaidi katika utengenezaji wa vyombo vya moto huku kampuni ya Sony wao wamejikita katika utengenezaji wa vifaa vya kielektroniki kama vile simu, kompyuta n.k.
Ukizingatia ukubwa wa sony katika mambo ya sensa, ni kwamba gari hilo linakuja likiwa na na kamera 45 na sense mbalimbali kwa nje ya gari na ndani ya gari huku zingine zikiwa ni mahususi kwa ajili ya kuzingatia usalama wa dereva.
Hata kwa upande wa software Honda na Sony wanatumia teknolojia ya chip kutoka kwa Qualcomm yaani Snapdragon Digital Chasis na teknolojia zingine nyingi ambazo ni za hali ya juu kutumika.
Kwa ushirika huu, sony wataifanya gari ya Ageela kuwa ni ya starehe sana maana ni wazi kwamba gari hii haitakosa kuja na filamu na magemu makali pengine magemu ya Playstation yatapatikana ndani ya gari hili.
Sony na Honda walitangaza mwaka jana kuwa wanaingia katika ushirika wa kutengeneza gari la umeme na ushirika huu wakaupa jina la Sony Honda Mobility ambapo kwa mara ya kwanza kabisa wanategemea kuanza kuuza magari haya ifikapo 2025.
Kwa sasa ushirika huo unasema unapendekeza wateja wake washiriki katika hatua zote za utengenezaji na uzalishaji wa gari hilo – japokua wengi hawataelewa hili.
Kwa sasa gari hizi zinazalishwa katika ofisi za Honda huko amerika, je unadhani gari hili litashindana vikali na magari mengine ambayo tayari yapo sokoni kama vile yale ya Tesla?
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la uwanja wa comment, je unadhani soko litalipokea vizuri gari hili na kuwa mshindani thabiti?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.