Utengenezaji wa Sony PS3 umefikia ukingoni hivyo basi usije ukashangaa huoni toleo lolote la PS3 dukani.
Sony ilibakiza tooleo moja tuu yaani lile yoleo la GB 500 ambalo ndilo lilikua linaendelea kuzalishwa, lakini kwa sasa zoezi hilo limefika ukingoni.
Mwanzoni mwa mwaka huu kampuni la Sony lilisema kabisa kuwa “Usafirishaji wa PS3 — kwenda nje ya nchi — utaisha hivi karibuni”
Maneno haya yalikua yanaligusa moja kwa moja toleo la PS3 GB 500 ambalo kwa kipindi hicho lilikua ndio toleo lenyewe tuu katika uzalishaji wa PS3.
PS3 ilitambulishwa rasmi mwaka 2006 na mpaka kufikia mwaka 2014 ndipo toleo liningene likaingia sokoni yaani PS4.
Lakini pia kama ni mfuatiliaji mzuri wa PS kumbuka moja kati ya nguzo zao ni kwamba wanatengeneza toleo moja la PS na wanadumu nalo kwa kipindi cha muda wa miaka 10 tuu. Hili limefikiwa sio….?
Kuacha kuzalisha matoleo ya PS3 haimaanishi chochote kwa PS3 ambazo zipo madukani na mikononi kwa watu bali inamaanisha kuwa kampuni haitatoa msaada mwingine wa kiufundi katika matoleo hayo ya PS3.
Kwa sasa kama ni mteja wa dhati ni bora kukimbilia katika toleo la PS4.