Kampuni ya Sony ipo katika hatua za mwisho za kuleta mrithi wa smartphone maarufu ya Xperia S, itakayotambulika kama Xperia SL.
Ingawa hutaziona kwa wingi smartphone za Sony kama za kampuni inayoongoza duniani ya Samsung, simu za Sony bila neno ‘Ericsson’ zinazidi kuwa na ubora katika maeneo mengi hii ni pamoja na ubunifu mzuri.
Xperia S ilikuwa simu ya kwanza kutolewa na Sony hapo mwenzi wa nne baada ya kununua asilimia zote zilizokuwa zinamilikiwa na kampuni ya Ericsson katika iliyokuwa kampuni iliyotambulika kama Sony-Ericsson.
Simu hii ya Xperia XL itakuwa na processor kasi zaidi ya 1.7 GHz dual-core processor, dhidi ya 1.5 GHz ilyokuwa kwenye Xperia S. Itakuwa na kioo cha inchi 4.3, pamoja na kamera ya megapixel 12.1 ambayo ni sawa kama ile ya Xperia S. Na kizuri zaidi itakuja na Android 4.0 maarufu kwa jina la Ice Cream Sandwich.
Smartphone hii kwa sasa inatajwa kwenye tovuti ya Sony kwenye kundi la “zinazokuja karibuni”. Pia tovuti inaonyesha orodha kamili ya sifa ya simu hii na picha, lakini bado hawajaweka bei na tarehe kamili itakapoingia sokoni.
No Comment! Be the first one.